MWENYEKITI WA TAS ARUSHA, GODSON MOLLEL MAZISHI YAKIENDELEA WAOMBOLEZAJI WAKIWA MBELE YA KABURI LA MAREHEMU HUYO
MKURUGENZI UTSS TZ, VICKY NTETEMA
MRATIBU WA POLISI ARUSHA, HAMIS WARIOBA
Na Idd Uwesu/Mpwaji Arusha yetu
Hatimaye
mazishi ya mtu mwenye ulemavu wa ngozi aliyeuwa kinyama wilayani
Arumeru mkoani Arusha miezi miwili iliyopita yamefanyika katika makaburi
ya Njiro jijini Arusha.
Mazishi
ya mlemavu huyo ambaye hakuweza kutambuliwa kutokana na kuchunwa ngozi
na kuondolewa baadhi ya viungo vyake yamefanyika chini ya usimamizi wa
Chama cha Maalbino Tanzania TAS na Shirika la Under the same sun
Tanzania
Mwanahabari wetu Idd UWESU anataarifa zaidi.
Akiongea
wakati wa mazishi hayo Mkurugenzi wa shirika la Under the same sun
Tanzania, Vicky Ntetema amesema kuwa jukumu la kuwalinda walemavu wa
ngozi nchini ni jukumu la kila mmoja na sio kuliachia jeshi la polisi
pekee au serikali. Amesema jamii ihakikishe walemavu hao wanalindwa na
kuthaminiwa kama binadamu wengine.
Ameongeza
kuwa mauaji hayo ya kinyama ni lazima yakomeshwe na kwamba wale wote
waliohusika na unyama huo kuhakikisha wanakamatwa na kufikishwa mbele ya
sheria. Amesema jamii ya kitanzania haina budi kuhakikisha inashirikana
na jeshi la polisi kuhakikisha watu hao wanakamatwa.
Insert 1……Mkurugenzi UTSS Tanzania, Vicky Ntetema
Nae
mwenyekiti wa mkoa wa Chama cha Maalbino Tanzania, Godson Mollel
amesema wanalaani vikali tukio hilo na kuitaka serikali na mashirika
mengine kukisaidia Chama chao ili kiweze kutembea maeneo mengi zaidi
kuendelea kuelimisha jamii hasa za vijijini kuhusu imani hizo potofu
ambazo ndizo chanzo kikubwa cha mauaji hayo
Insert 2……Mwenyekiti TAS Arusha, Godson Mollel.
Kwa
upande wa Jeshi la polisi, Mrakibu wa Polisi mkoa wa Arusha Hamis
Warioba amesema Jeshi hilo hivi sasa linaendelea na uchunguzi na kwa mba
halitasimama mpaka lihakikishe watu waliohusika na mauaji hayo
wanakatamatwa na kufikishwa mbele ya sheria.
Insert 3……. Mrakibu wa Polisi mkoa wa Arusha, Hamis Warioba
Mwili
wa mlemavu huyo uliokotwa tarehe 29 mwezi mei mwaka huu pembezoni mwa
nyumba ya mkazi mmoja wilayani Arumeru. Mazishi hayo pia yalihudhuriwa
na Mariamu Staford mlemavu wa ngozi ambaye alikatwa mikono yake
alipovamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwao huko Ngara.CREDITS: ARUSHA YETU BLOG
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)