Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Dk.
Faustine Ndungulile akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo na viongozi
wakuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati kamati yake
ilipofanya ziara katika makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo
Kurasini,jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Mh. Deogratius
Mtukamazina (kulia) akitoa salamu ya Bodi yake kwa Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyofanya ziara yale leo kwenye
makao makuu ya Mfuko huo yenye lengo la kujifunza mambo mbali mbali
yanayofanya na Mfuko huo.Wengine pichani ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati
Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Dk. Faustine Ndungulile,Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii,Mh. Dk. Hussein Mwinyi,Naibu Waziri wa
Afya, Dk. Sirra Umbwa,Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(TAMISEMI),Mh. Majaliwa K. Majaliwa.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii,Mh. Dk. Hussein Mwinyi akizungumza na
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyofanya ziara
yale leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo yenye lengo la kujifunza
mambo mbali mbali yanayofanya na Mfuko huo.
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na Mbunge wa Jimbo la
Korogwe Vijijini,Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu akisalimia
wadau.
Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla nae akisalimia wadau.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Ndg. Emmanuel Humba
akitoa maelezo mafupi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii.
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii wakifuatia
kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa ukumbini hapo.
Wakurugenzi wa NHIF.
Wajumbe wa Bodi ya NHIF.
Meneja
wa Idara ya Uanachama wa NHIF,Bi. Ellentruder Mbogoro akielekeza jambo
kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii
walipotembelea makao makuu ya Mfuko huo,Kurasini jijini Dar es Salaam
leo.
Afisa
Nyaraka wa NHIF,Erastus Msigwa akiwaonyesha Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii moja ya mafaili ya Wanachama wa
Mfuko huo yaliyohifadhiwa kwenye Masanduku ya Kisasa yanayotumia mfumo
wa Umeme.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii wakipata maelezo ya
namna ya uhifadhi wa Nyaraka kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Sehemu ya Masanduku hayo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)