Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo Dkt. Finella Mukangara,
---
Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo Dkt. Finella Mukangara,amenusurika
kifo katika ajali ya gari iliyotokea leo Igunga mkoani Tabora wakati
akiwa safarini kuelekea Mwanza akitokea Dodoma.
Gari
la Waziri Dk. Mukangara linadaiwa kupinduka wakati dereva wake
akijaribu kulipita roli la mizigo na kutaka kugongana uso kwa uso na
basi la Green Sta lililokuwa likitokea Mwanza.
Waziri, Msaidizi wake na dereva walipata majeraha na kutibiwa katika Hospitali ya Nzega Mkoani Tabora
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)