Moja
kati ya magari ya kampuni ya CFAO Motors Group yaliyokuwa yakiendeshwa
na wateja kutoka kampuni tofauti likikatiza katika mabonde wakati wa
Ride & Drive yakiwemo Nissan, Benz, VW ‘AMAROK’ na Suzuki kujaribu
ubora wake.
Katika msafara wa It’s Ride &ra huo piwa walikuwapo Kinamama ambao nao pia walishiriki.
Msafara
wa magari tofauti ya kampuni ya CFAO Motors Group, yakiendeshwa na
wateja kutoka kampuni tofauti wakati wa Ride & Drive yakiwemo
Nissan, Benz, VW ‘AMAROK’ na Suzuki yakichanja mbuga kwenye mabonde na
milima kujaribu ubora wake.
Sales
Representative wa CFAO Motors Magdalena Mpeku (wa pili kulia) na Tender
Manager Bw. Marco Kahabi wakizungumza na kubadiliashana mawazo na
baadhi ya wageni waalikwa baada ya zoezi la Ride & Drive.
Mkurugenzi Mkuu wa CFAO Motors Uganda Bw. Eric Ruiz akibadilishana mawazo na Meneja Masoko Mpya wa CFAO Motors Tharaia Ahmed.
********************************
********************************
Na Mwandishi wetu
Kampuni
maarufu ya kuuza na kusambaza magari nchini Tanzania ya CFAO Motors kwa
mara nyingine imewapa fursa wateja wake kuyajaribu kwa kuyaendesha
magari wanayoyauza na gari mpya aina ya Volks Wagon katika viwanja vya
maeneo ya Coco beach.
Wateja
hao kutoka kampuni mbalimbali wamepata nafasi ya kupakia na pia
kuyaendesha magari mapya yanayoingizwa hapa nchini na kampuni hiyo ili
kujua upya na uimara wa magari hayo hivyo kuweza kuchagua magari bora ya
kununua.
Akizungumza
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed amesema kampuni hiyo
imechagua viwanja hivyo kwa kuwa vina sehemu zenye mawe, miinuko na
barabara korofi ili wateja wao waweze kuthibitisha uimara wa magari
yanayouzwa na kampuni hiyo.
Naye
Mkurugenzi mpya wa kampuni mpya ya Alliance Motors Bw. Alfred Minja
amesema kampuni yake ambayo ni moja ya makampuni ya CFAO Motors Group
imeingiza magari mapya aina ya Volks Wagon yakiwemo ‘Amarok’ ikiwa ni
katika kuwapatia watanzania nafasi ya kuchagua gari bora wanalolipenda
kwa gharama nafuu.
Nao
baadhi ya wateja waliopata nafasi yak u-‘Ride and Drive’ wamesifia
ubora na upya wa magari hayo na kuhimiza watanzania na kampuni mbali
mbli kununua gari hizo.
Dereva
wa siku nyingi na mwanajeshi wa zamani Bw. Issa Swalehe amesema kuanzia
gari kubwa aina ya ‘Benzi Zitros’ ni nzuri hasa katika sehemu
sizizopitika kirahisi na gia zake zinaingia kirahisi kama unavyoendesha
gari ndogo.
Kampuni
ya CFAO Motors ambayo kwa sasa imefungua kampuni ya Alliance Motors
itakayokuwa chini ya Bw. Alfred Minja na kuuza aina tofauti za magari ya
‘Volkswagon’, Nissan, Benzi na mengineyo hufanya tukio kama hilo la
kutoa fursa wa wateja wake ku-‘feel’ ubora wa magari hayo mara tatu kwa
mwaka.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)