Precision Air wazindua safari ya Dar-Lusaka kupitia Lubumbash - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Precision Air wazindua safari ya Dar-Lusaka kupitia Lubumbash

 Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air, Alfonse Kioko akiteremka katika ndege na Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Judith Kangoma baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Kenth Kaunda mjini Lusaka Zambia leo.
 Kioko akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Zambia
 Bendera zikiashiria ushirikiano kati ya Zambia na Tanzania
 MD wa Precision Air Alfonse Kioko akiongozana na Naibu Waziri wa Uchukuzi Zambia
 Abiria na watumishi wa Precision Air wakiwa Lusaka
 Abiria wa kwanza wa safari ya ndege PW 704 ya Shirika la Ndege la Precision Air wakipokelewa katika Uwanja wa Kimataifa wa Keneth Kaunda mjini Lusaka leo baada ya kuwasili salama wakitokea jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wakipiga picha ya pamoja mjini Lusaka Zambia baada ya kuwasili salama
Viongozi wakijadili jambo. Kushoto ni Balozi wa tanzania nchini Zambia.
 Cabin Crew hiyo nayo
Marubani waliofanikisha ndege hiyo PW 704 kufika uwanja wa Keneth Kaunda mjini Lusaka zambia wakilamba picha.

 Shirika la ndege la Precision Air la jijini Dar es Salaam, Tanzania leo limezindua safari yake mpya ya kwenda Lusaka, Zambia kupitia Lubumbash nchini Congo DRC.

Kuanza kwa safari hiyo mpya hii leo kumepokelewa kwa shangwe na wafanyabiashara wa nchi za Zambia na Congo na wale wa Tanzania maana sasa hawatalazimika kupitia Nairobi wala Johannesburg  Afrika Kusini wakitaka kwenda Lusaka ama Dar es Salaam.

Kwakutumia ndege PW 704 hivi sasa safari ya Dar es Salaam hadi Lusaka itachukua saa 2 na robo badala ya zaidi ya saa kumi ambazo abiria alikuwa akizitumia awali kwa kupitia Nairobi.

Safari hiyo mpya ya Precision Air imezinduliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, John Thomas James Mngodo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages