Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela akiwa anaapa kiapo cha utiifu mbele ya mkuu wa mkoa wa arusha Magesa Mulongo leo
Akuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa akiwa anakula kiapo cha uaminifu mbele ya mgeni rasmi
Wakuu wa wilaya wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha (picha zote na Gladness Mushi-Arusha
Katika jiji la Arusha leo wakuu wapya wilaya wameapishwa ambapo Mkuu
wa mkoa wa Arusha magesa mulongo amewaotaka wasiliwe sifa na badala yake
wahakikishe kuwa wanajikita zaidi katika kutatua kero za wananchi.
Mbali na hayo aliwataka washirikiane na Madiwani katika kutatua
tatizo la hati chafu ndani ya halmashauri kwa kuwa kati ya halmashauri
zote jijini hapa iliyo na hati safi kidogo ni halmashauri ya Meru pekee
Pia aliwataka wakuu hao kuhakikisha hawapigwi chenga na sheria mbalimbali hasa za vijiji na ile ya asilimia ishirini kwa kila lkijiji kwa kuwa kwa sasa halmashauri zinakwepa sheria hiyo na hali hiyo inapelekea wenyeviti wa vijijiji kuwa katika hali nghumu ya kiutendaji
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)