Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika lilivyorindima Uturuki - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika lilivyorindima Uturuki


Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward akiwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.

Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (kushoto) akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Jamhuri ya Uturuki (Idara ya Habari na Maelezo), Murat Karakaya iliyotolewa kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan, baada ya kuwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc akifungua mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Mhariri wa Habari wa gazeti la Nipashe Jumapili, Beatrice Bandawe(wa pili kushoto) akifuatilia mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita.
Mkurugenzi wa Raia Mwema aliyepata pia kuwa MhaririMtendaji wa gazeti hilo na Kampuni ya New Habari Corporation 2006, John Bwire (kushoto) na Mhariri wa Makala wa Habari Leo, Selemani Nzaro wakifuatilia mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu Uturuki, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Profesa, Dk. Mohamed Bakari, raia wa Kenya anayefundisha Chuo Kikuu cha Fatih nchini Uturuki, akipokea tuzo maalumu iliyotolewa kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc baada ya kuwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Afrika ya Leo: Sera za Siasa, Uchumi na Mambo ya Nje' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia wakati Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (mbele kwenye video) akiwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu Uturuki, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages