MNYAMA AIBUKA KIDEDEA KWA MAGOLI 2 KWA BILA DHIDI YA ES SETIF - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MNYAMA AIBUKA KIDEDEA KWA MAGOLI 2 KWA BILA DHIDI YA ES SETIF

Mchezaji Emanuel Okwi wa Simba akiruka juu juu kuupiga kwa kichwa mpira katikati ya mabeki wa timu ya Es Setif katika mchezo wa Kombe la Shirikisho unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii, Mpira umekwisha Simba imeshinda magoli mawili yaliyofungwa na wachezaji Emmanuel Okwi goli la kwanza na Haruna Moshi "Boban" goli la pili. Mashabiki wa Simba wanashangilia kwelikweli huku na baada ya Simba kufunga magoli mwashabiki wa Yanga walianza kuondoka uwanjani kabla ya mpira kuisha ni kazi kwelikweli.
 Mchezaji wa timu ya Simba Emmanuel Okwi akiruka juu juu katikati ya mabeki  watimu ya ES Setif wakati timu hizo zilipopambana katika kombe la Shirikisho kwenye uwanja wa Taifa leo.
Mchezaji wa Simba Amir Maftaha akikabana na mchezaji wa timu ya ES Setif ya Algeria katika mchezo wa kombe la Shirikisho.Picha Kwa Hisani ya http://mamapipiro.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages