Mkuu
wa Wilaya ya Kigoma John Mogella akifunguwa Mkutano wa Tano wa Mamlaka
ya Ziwa Tanganyika,kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mkutano huo
umehusisha Nchi za Tanzania,Zambia,Burundi na Congo kwenye Hotel ya Lake
Tanganyika
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Terezya Huvisa akimsikiliza
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika Bw. Dk Henry Mwima
wakati wa Mkutano wa Tano wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika uliofanyika
kwenye Hotel ya Lake Tanganyika Mkoani Kigoma
Mawaziri
wa Nchi za Mamlaka ya Ziwa Tanganyika wakiangalia Ngoma [pichani haipo]
wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika
uliofanyika kwenye Hotel ya Lake Tanganyika Mkoani Kigoma.Picha na Ali
Meja
---
Na Lulu Mussa-Kigoma
Mkutano
wa Tano wa Mawaziri wa Mamlaka ya ziwa Tanganyika umefanyika leo mkoani
Kigoma, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya mkataba uliounda mamlaka
hiyo.
Katika
hotuba yake ya ufunguzi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira) Dk. Terezya Huvisa amesema kuwa ili kulinusuru Ziwa
Tanganyika jitahada za Nchi zote nne ni muhimu katika kukabiliana na
changamoto zinazolikabili ziwa hilo kwa sasa kwa kutumia fursa zilizopo.
Amezitaja
changamoto hizo kuwa ni pamoja na uchafuzi mkubwa wa mazingira ikiwa ni
pamoja na kujaa kwa taka za majumbani na zile za viwandani, uvuvi
haramu kutokana na ongezeko la watu, kilimo na ufugaji usio endelevu.
Hata hivyo Waziri Huvisa amewakumbusha wajumbe wa Mkutano huo kuwa Ziwa
Tanganyika linaunganisha Nchi zote nne badala ya kuzitenganisha, hivyo
ni muhimu kuwa na mikakati endelevu ya kuhifadhi ziwa hilo.
Miongoni
mwa maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano huo ni pamoja na Utekelezaji
wa Mpango Mkakati wa Kitaifa ambao kwa sasa unafanya kazi katika nchi
zote pamoja na Mkakati wa kukusanya fedha kwa ajili ya kuwa na usimamizi
endelevu wa Ziwa Tanganyika baadaya ya mwaka 2013 ambapo fedha za
wafadhili zitafikia kikomo.
Katika
Mkakati huo wa kukusanya fedha Nchi zote nne zimetia saini makubaliano
ya kuchangia fedha ili hifadhi ya Ziwa hilo iwe endelevu, ikiwa ni
pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Mkutano
huo umefanyika Tanzania kwa mara ya pili, mkutano mwingine kama huo
ulifanyika jijini Dar es Salaam mwaka 2007. Mamlaka hiyo ya Ziwa
Tanganyika inaundwa na nchi za Zambia, Burundi, Congo (DRC) na mwenyeji
Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)