Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) limekuwa na kawaida ya kutoa fursa za mafunzo ya makada wake ndani na nje ya Tanzania.
Dira ya BAVICHA ni kuona vijana ni nguvu ya mabadiliko ya kidemokrasia kwa maendeleo yao na ya taifa.
Kwa awamu hii BAVICHA limepanga kupeleka kada wake kwenye mafunzo ya
wiki moja kwa wanasiasa vijana (Summer School) Berlin, nchini Ujerumani.
BAVICHA inawaalika vijana wa CHADEMA watakaopenda kushiriki mafunzo
hayo kutuma barua ya maombi ya kushiriki, ikiambatana na wasifu
unaojitosheleza (CV).
BAVICHA inahimiza vijana kutuma maombi kwa kuwa taarifa za waombaji
zitahifadhiwa katika kumbukumbu (data bank) kwa ajili ya fursa nyingine
zinazojitokeza.
Mwombaji pia anatakiwa ataje mawasiliano yake, namba ya kadi yake ya
uanachama, tarehe ya kujiunga na chama na aeleze ushiriki wake ndani ya
BAVICHA na Chama pamoja na matarajio yake ndani ya BAVICHA na CHADEMA
kwa ujumla.
Maombi yatumwe kwa
Katibu Mkuu wa BAVICHA kupitia
bavicha@chadema.or.tz na nakala info@chadema.or.tz
kabla ya tarehe 10/03/2012.
Dhima ya BAVICHA ni kuwezesha uwepo wa sera sahihi , uongozi bora na
kujenga oganaizesheni thabiti ya vijana kwa maendeleo endelevu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)