Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa na Mkuki na Vazi rasmi la heshima la Kabila la Wanyakyusa, baada
ya kukabidhiwa wadhfa huo na wazee wa Kabila la Wanyakyusa wa Kijiji cha
Mbambo Wilaya ya Rungwe, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Mbeya jana
Februri 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Mkuki
kutoka kwa mwakilishi wa Wazee wa Kabila la Wanyakyusa wa Kijiji cha
Mbambo Wilaya ya Rungwe, Ambakisye Mwakatobe, ikiwa ni ishara ya
kumkabidhi wadhfa wa kuwa Mzee wa Kabila la Wanyakyusa, wakati alipofika
katika Kijiji hicho kuwahutubia akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa
Mbeya jana Februari 26, 2012. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha
Bilal.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiweka jiwe la msingi katika chanzo cha mradi wa maji ya umwagiliaji
katika Kijijji cha Kisegese, Wilaya ya Rungwe mtaro wenye urefu wa
Kilomita 7, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Mbeya jana
Februari 26, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, wakiangalia Mpunga katika eneo la
Shamba Darasa, lililopo Kijiji cha Kisegese Wilaya ya Rungwe, wakati
akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Mbeya, jana Februari 26, 2012.
Makamu
Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitembelea na kukagua mtaro wa kupitishia maji ya umwagiliaji katika
Kilimo mradi uliopo katika Kijiji cha Kisegese, wakati akiwa katika siku
yake ya mwisho ya ziara yake ya Mkoa wa Mbeya jana Februari 26, 2012.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)