FFU NGOMA AFRICA BAND KUVAMIA INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL TUBINGEN GERMANY JUMAMOSI YA TAREHE 16/7/2011 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

FFU NGOMA AFRICA BAND KUVAMIA INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL TUBINGEN GERMANY JUMAMOSI YA TAREHE 16/7/2011


             Mabakuli ya "Supu ya Mawe" uwanjani kila moja na lake!
    
Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU,kinatarajiwa kutumbuiza
 jukwaani tena katika onyesho kubwa la aina yake African Internationals Festival,mjini Tübingen,ujerumani siku ya jumamosi 16.julai 2011.
FFU hao wamziki pia wamepakua jikoni wimbo mpya uliobeba jina "SUPU YA MAWE" wimbo wenye ujumbe
mahusus kwa walimwengu ,ambao kwa sasa unasikia katika kambi ya FFU  at www.ngoma-africa.com, wimbo huo utunzi wake kamanda Ras Makunja akiimba kwa kushirikiana na Christian Bakotessa aka Chris-B aka "Mshenzi" wa gitaa la solo.Wimbo huo "Supu ya Mawe"
ujumbe uliomo katika wimbo huo unaonekana kuwa na nguvu na vitamin zote za maisha kuliko kikombe cha dawa.
kutokana na taarifa la gazeti moja la kimataifa hili  http://www.africa-news.eu/entertainment/44-entertainment/2815-welcome-to-international-african-festival-in-tubingen-germany.html   bendi hiyo maarufu inazidi kupata umaarufu na kujizolea washabiki kiaina yake katika kila kona.
Usikose kuwasikiliza
 at www.ngoma-africa.com hili nawe upate bakuli la "Supu ya Mawe"

soma habari zaidi:

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages