Mmoja wa Msukule uliowahi kukamatwa.
Pamoja na Serikali kuendelea
kuelimisha jamii mkoani Shinyanga juu ya imani potofu za kishirikina
zinazopelekea kutokea kwa mauaji lakini bado wananchi wanaendelea na
vitendo hivyo ambapo watu wawili wameuawa kwa kukatwakatwa mapanga na
kisha kuchomwa moto hadi kufariki dunia.
Akizungumza na waandishi wa Habari mkoani humo Kamanda wa polisi Diwani Othuman amesema mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Khamisi mkazi wa kijiji cha Mishepo Shinyanga Vijijini ameuwawa baada ya wananchi kujichukulia sheria mikononi kwa kumpiga mawe na kuchapwa viboko, kisha kumkataka mapanga hali iliyopelekea kifo chake.
Amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo,inadaiwa kuwa marehemu aliiiba televisheni, baiskeli, ambapo mhusika wa vitu hivyo hajajulikana hivyo polisi wanaendelea na uchunguzi.
Aidha Katika tukio la pili lililotokea kijiji cha Nanga Wilayani Bariadi mwanaume mmoja anayeitwa Nira Salu mwenye umri wa miaka 41 amekutwa amekufa kwenye chooni huku ikidaiwa kwamba chanzo ni kuzidiwa na Ulevi wa pombe aliyokunywa kupita Kiasi.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)