Pages

NMB YAMWAGA MISAADA KWA TIMU ZA JWTZ, WANAJESHI WATOA TAMBO


Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo kutoka Benki ya NMB, Salie Mlay (kushoto) akimkabidhi moja ya jezi zilizokabidhiwa Kanali Damian M. Majare(katikati).
Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo kutoka Benki ya NMB, Salie Mlay (kushoto) akimkabidhi mipira Kanali Damian M. Majare (katikati).


TIMU za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zimepokea msaada wa vifaa vya michezo kwa ajili ya kuboresha timu zao mbalimbali zinazoshiriki katika Ligi Kuu Bara na michuano ya mbalimbali ya majeshi.



Msaada huo wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 10 umetolewa na Benki ya NMB Tanzania, leo Jumatatu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Kanali Damian M. Majare ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Kanda ya Ngome.



Akizungumza katika hafla hiyo, Kanali Damian M. Majare alisema vifaa hivyo vitawawezesha kujiimarisha kukabili michuano ya majeshi inayotarajiwa kuanza mapema mwakani.




Kwa upande wake, Kanali Erasmus Bwegoge ambaye ni Mkurugenzi wa Utimamu wa Mwili, Michezo na Utamaduni kutoka JWTZ amesema timu zitakazonufaika na msaada huo ni pamoja na timu za Ruvu Shooting, JKT Tanzania, Green Warriors, Mlale JKT ya Songea, Mgambo Shooting na baadhi ya timu ambazo zinashiriki Ligi Daraja la Kwanza.



Naye Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo kutoka Benki ya NMB, ambao ndiyo wametoa msaada huo, Salie Mlay amesema kuwa wanalenga kuona Timu za JWTZ zikiongeza mwamko katika mashindano mbalimbali hususan mashindano ya majeshi ili waweze kuliwakilisha taifa  kikamilifu.
Meza kuu ilivyoonekana mbele.


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)