Pages

NMB IMEUGANA NA 'OPEN KITCHEN' KUTOA SEMINA KWA AKINA MAMA WAJASIRIAAMALI

 Ofisa Biashara wa Benki ya NMB, Bi. Beatrice Mwambije (katikati) akiwasilisha mada kwenye kongamano la mafunzo kwa akinamama wajasiriamali 'Open Kitchen' lililodhaminiwa na Benki ya NMB. 
 Ofisa Biashara wa Benki ya NMB, Bi. Beatrice Mwambije (wa kwanza kulia) akifafanua jambo juu ya huduma za NMB kwa baadhi ya washiriki kwenye kongamano la mafunzo kwa akinamama wajasiriamali 'Open Kitchen' lililodhaminiwa na Benki ya NMB. 
 Sehemu ya washiriki kwenye kongamano la mafunzo kwa akinamama wajasiriamali 'Open Kitchen' lililodhaminiwa na Benki ya NMB wakifuatilia mada anuai. 

 Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya NMB (katikati aliyesimama) akigawa fomu za taarifa za NMB kwenye kongamano la mafunzo kwa akinamama wajasiriamali 'Open Kitchen' lililodhaminiwa na Benki ya NMB. 


Mwanasaikolojia Lisbeth Mhando (kulia) akiwasilisha mada kwenye kongamano la mafunzo kwa akinamama wajasiriamali 'Open Kitchen' lililodhaminiwa na Benki ya NMB. 



Mmoja wa akinamama wajasiriaamali waliofanikiwa baada ya kukuzwa na Benki ya NMB kimtaji akiwasimulia wenzake namna Benki ya NMB ilivyomsaidia kukuza biashara zake.


BENKI ya NMB imedhamini kongamano la mafunzo kwa akinamama wajasiriamali waliokutana jana kupata mafunzo anuai ya kijasiriamali yaliyolenga kumuinua mwanamke kibiashara.

Kongamano hilo lilifanyika jana jijini Dar es Salaam ambapo zaidi ya kinamama 200 kutoka jijini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa walinufaika na mada zilizolenga kumnyanyua mwanamke mjasiriamali.

Akizungumza katika kongamano hilo, Ofisa Biashara wa NMB, Bi. Beatrice Mwambije aliwataka akinamama kujenga mazoea ya kukuza vipato vyao kwa kupunguza gharama zisizo za msingi katika maisha.

Alisema matumizi yasiyo ya lazima yamekuwa yakipoteza kipato cha akinamama na kujikuta wanashindwa kukuza biashara zao, hivyo kuwashauri kuanza kubana matumizi yasiyo ya lazima.

"...Tujifunze kuongeza kipato chetu kwa kupunguza gharama zisizo na ulazima, tujitaahidi kupata elimu ya kutosha hata kabla ya kuomba mkopo katika biashara zetu," alisema Bi. Mwambije.

Aliwashauri kuitumia NMB katika kuendeleza biashara zao kwa mikopo kwani maofisa wa benki hiyo hutoa elimu na ushauri wa kutosha kabla ya kumpa mkopo mfanyabiashara ili usije kuwa mziko kipindi cha kurejesha.

Aidha aliongeza kuwa mtaji wa biashara unaweza kuwa mali yoyote au mali kauli kwa wajasiriamali waaminifu hivyo kuwashauri wasiogope kujitokeza kufanya biashara kwa wale ambao bado hawajaingia rasmi kwenye biashara.

Kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu; Wanawake tuna nia, tunasababu, na sasa tunajiwezesha ambalo lilitoa nafasi kwa akinamama kupata mafunzo toka kwa wajasiriamali waliofanikiwa ambao pia walipata fursa ya kupata mikopo inayotolewa na Benki ya NMB.

Mwanamama mjasiliamali (kushoto) akiuliza swali kwa watoa mada (hawapo pichani).

Mwanasaikolojia Lisbeth Mhando akiwaelekeza akinamama wajasiriamali namna ya kupunguza asira au furaha iliyopitiliza kwa kutumia pumzi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)