Pages

NMB YAKABIDHI MABATI 312 SEKONDARI YA WASICHANA GALIJEMBE, MBEYA

Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Bi. Vicky Bishubo (wa pili kulia) akimkabidhi msaada wa mabati 312 yenye thamani ya shilingi milioni 10 Naibu Waziri Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Mary Mwanjelwa (wa pili kushoto). NMB imetoa mabati hayo kwa ajili ya kuezeka Shule ya Sekondari ya Wasichana Galijembe iliyopo mkoani Mbeya.


Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Bi. Vicky Bishubo (kushoto walioshikana mikono) akimkabidhi msaada wa mabati 312 yenye thamani ya shilingi milioni 10 Naibu Waziri Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Mary Mwanjelwa (kulia).

Naibu Waziri Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Mary Mwanjelwa (wa pili kushoto walioinama) akiangalia moja ya nembo zilizopo kwenye mabati aliyokabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Bi. Vicky Bishubo kwa ajili ya kuezeka Shule ya Sekondari ya Wasichana Galijembe iliyopo mkoani Mbeya.

Naibu Waziri Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Mary Mwanjelwa akizungumza katika hafla hiyo.


BENKI ya NMB imekabidhi msaada wa mabati 312 yenye thamani ya shilingi milioni 10 ikiwa ni kwa ajili ya kuezeka Shule ya Sekondari ya Wasichana Galijembe iliyopo mkoani Mbeya.

Msaada huo umekabidhiwa leo shuleni hapo na Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa Benki ya NMB, Bi. Vicky Bishubo na kupokewa na mgeni rasmi katika hafla ya makabidhiano, Naibu Waziri Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Mary Mwanjelwa.

Akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo, Bi. Bishubo alisema elimu bora huambatana na mazingira bora ya kutolea elimu hiyo hivyo wadau wana kila sababu kusaidia uboreshaji mazingira hayo.

Aliongeza kuwa NMB kama wadau inazidi kuwa karibu na jamii inayoizunguka kwa kuboresha mazingira ya wanafunzi shuleni kwa kusaidia kwa njia mbalimbali. 

"..Kufanikisha hili tumekabidhi mabati 312 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuezeka shule ya sekondari ya wasichana Galijembe-Mbeya ikiwa ni kuboresha maazingira ya elimu kwa wanafunzi," alisema Bi. Bishubo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)