Pages

UKOSEFU ELIMU YA UJASIRIAMALI WAKWAMISHA MALENGO YA WATANZANIA-SPIKA NDUGAI

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akizungumza wakati akifungua Kongamano la wateja wa Benki ya NMB lililofanyika jijini Dodoma, likilenga kutoa elimu ya biashara.
Afisa Mkuu wa Mikopo Benki ya NMB, Tom Borghols kizungumza na washiriki wa mkutano huo.


Sehemu ya washiriki katika kongamano la wateja wa Benki ya NMB lililolenga kutoa elimu ya biashara.


SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao kutokana na kutokuwa na elimu ya ujasiriamali na hivyo pesa wanazo kopa kushindwa kuzifanyia malengo waliyokusudia.Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo, Mh. Ndugai ameitaka Benki ya NMB kuhakikisha inatoa elimu ya ujasiriamali ili kuwawezesha wananchi kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla. Spika ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati alipokuwa akifungua kongamano la wateja wa Benki ya NMB lililolenga kutoa elimu za biashara na namna nzuri ya kutunza fedha zao.
Aidha Spika ameipongeza Benki ya NMB kwa kuandaa mafunzo yakuwajengea uwezo wafanyabiashara kwani elimu hiyo ni muhimu katika kuwajengea uwezo wafanyabiashara na wananchi juu ya umuhimu wakulipa kodi na kujenga mahusiano mazuri na wadau na taasisi mbalimbali za umma.
Naye Afisa Mkuu wa Mikopo, Tom Borghols amesema kuwa hivi sasa benki hiyo imeboresha utoaji wa huduma zake ikiwa ni pamoja na kuondoa baadhi ya masharti hasa ya hati ya nyumba kwa wateja wanaotaka kukopa mikopo mikubwa na pamoja na kumpa mamlaka meneja wa tawi kuidhinisha mkopo kwa mteja hadi wa shilingi milioni 50.
Jumuiko hilo lililoandaliwa na benki hiyo ya nmb limewashirikisha jumla ya wajasiriamali 300 wa mkoa wa Dodoma ambao ni wafanyabiashara wa club za wafanyabiashara (NMB Business Club) wa Benki ya NMB jijini hapa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)