Pages

WAZIRI JAFO ATOA RAI KWA VIONGOZI WA MKOA WA SINGIDA KUCHUKUA HATUA KUBORESHA UPATIKANAJI ELIMU BORA

Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Mkoani Singida wakiwa kwenye maadamano ya maadhimisho ya juma la elimu Kitaifa yaliyozinduliwa wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida.
Vingozi wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) pamoja na wadau mbalimbali wa elimu, serikali na taasisi binafsi wakiwa kwenye maadamano ya maadhimisho ya wiki ya elimu Kitaifa yaliyozinduliwa wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida.
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Eng. Jackson Masaka akiwakaribisha wageni na washiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya elimu Kitaifa yaliyozinduliwa wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi akizungumza wakati wa wiki ya elimu Kitaifa yaliyozinduliwa wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida.
Mbunge wa Mkalama, Mh. Allan Mkumbo akiwakaribisha wageni rasmi wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu iliyoratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Ikishirikiana na wadau wa elimu zikiwamo taasisi binafsi.
Mmoja wa wanafunzi akitolea ufafanuzi wakati ya wiki ya elimu iliyoratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) Ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, serikali na taasisi binafsi hapa nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi akikagua baadhi ya bada wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu Kitaifa yaliyozinduliwa wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida yaliyoratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, serikali na taasisi binafsi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi(kulia) akizungumza jambo wakati wa mabanda ya elimu katika maadhimisho ya wiki ya elimu Kitaifa yaliyozinduliwa wilayani Mkalama, Mkoa wa Singida yaliyoratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, serikali na taasisi binafsi.


* Mtandao wa Elimu Tanzania yapigania haki ya mtoto kupata elimu bora kufikia malengo 

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Suleiman Jafo ametoa rai kwa viongozi wa Mkoa wa Singida na Wilaya ya Mkarama kuchukua hatua za maksudi kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto ikiwemo kupiga vita mimba na ndoa za utotoni.

Jafo aliyekuwa mgeni maalumu ametoa kauli hiyo jana wakati akizindua Maadhimisho ya  Juma la Elimu ambayo kitaifa yamefanyika wilayani Mkalama mkoani Singida Mei 14 mwaka huu hadi Mei 18 mwaka huu ambapo mgeni alikua Mkuu wa Mkoa Dk.Rehema Nchini.

"Nitoe rai kwa viongozi wa Mkoa wa Singida na Wilaya ya Mkalama kuchukua hatua za makusudi kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto ikiwemo kupiga vita mimba na ndoa za utotoni, upatikanaji wa chakula shuleni na ushiriki wa wazazi na jamii kwa ujumla kuwajibika,"amesisitiza.

Taarifa kwa vyombo vya habari imesema kuwa maadhimisho hayo ambayo kitaifa yamezinduliwa mkoani humo ni kwamba kampeni ya wiki ya elimu duniani huadhimishwa kati ya Aprili na Mei kwa kila mwaka. Kwa Tanzania maadhimisho hayo huratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Ikishirikiana na wadau wa elimu zikiwamo taasisi binafsi.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Cathleen Sekwao amesema malengo ya maadhimisho hayo kuhamasisha, kutetea na kushawishi maslahi ya watoto kupata elimu bora ili kufikia malengo yao. 

Amefafanua sababu iliyochangia maadhimisho ya juma la elimu Kitaifa kufanyika wkuwa ya mwisho kimkkoa katika matokeo ya darasa la saba 2017, hivyo wamekutana huko kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja kutatua matatizo yaliyosababisha kutokufanya vizuri.

Kwa upande wa Dk.Nchimbi amesisitiza umuhimu wa kutambua changamoto kwa pamoja na umuhimu wa wadau kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua changamoto hizo. Akielezea kusikitishwa kufanya vibaya katika matokeo ya elimu ya msingi katika Mkoa wa Singida, alielezea mfanikio yaliyopo katika sekta ya elimu ikiwemo ongezeko la idadi ya uandikishaji wa wanafunzi elimu ya msingi, ugawaji wa vitabu na ongezeko la fedha katika sekta ya elimu.

Mgeni maalum, mgeni rasmi, viongozi mbalimbali, wanafunzi na wanachi kwa ujumla wamepata nafasi ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho ya kazi za wadau wa elimu ikiwemo TENMET, TWAWEZA, Right to Play, HakiElimu, Camfed, CBP, VSO, ADD International, AFRIWAG na REPPS.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)