Pages

MSANII DIAMOND AZINDUA WIMBO WA COLOURS KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

Msanii Diamond akipagawisha mashabiki wa Soka waliohudhuria katika Uzinduzi wa wimbo wa Colours maalum kwa ajili ya kombe la dunia 2018 linalofanyika nchini Urusi.
Mkurugenzi wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios akiongea machache kuhusu hafla hiyo,(kushoto) ni Meneja wa Coca-Cola nchini, David Karamagi.
Mkurugenzi wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios akikata keki wakati wa hafla hiyo.
Msanii Diamond akisalimiana na Mameneja Waandamizi wa Coca-Cola.
Msanii Peter Msechu na bendi yake wakipagawisha mashabiki wa soka waliohudhuria katika uzinduzi wa wimbo maalum alioshirikishwa msanii Diamond utakaosheresha Kombe la Dunia 2018.

Na Mwandishi Wetu.

MSANII wa Bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewapagawisha vilivyo mashabiki wake wakati akiimba wimbo maalum utakaosherehesha Kombe la Dunia 2018 wimbo uitwao Colours nyimbo aliyoshirikiana na Jason Derulo, katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo, alisema kampuni ya Coca-Cola Tanzania ni moja ya mdhamini wa mashindano hayo makubwa ya soka duniani na inayofuraha kwa msanii kutoka Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano hayo na kwamba anaimani watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya mashindano.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)