Pages

MKAZI WA NEWALA,SHAKILA AMRI ASHINDA MILIONI 140 SIKU YA MAMA DUNIANI

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TatuMzuka, Sebastian Maganga akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema jana jijini Dar,wakati wa kumtambulisha mshindi Shakila Amri Nyani aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 140 huku 'akimbust' Mama yake kwenye sehemu ya usindi wake kwa kumpa kiasi cha shilingi milioni 30.

  Shakila
Amri Nyani aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 140 huku akifafanua zaidi kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani),namna alivyofanikiwa kushinda kitita hicho cha TatuMzuka,aidha kufuatia ushindi huo Shakila pia 
'alimbust' Mama yake kwenye sehemu ya ushindi wake kwa kumpa kiasi cha
shilingi milioni 30.


 
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano wa TatuMzuka, Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi mshindi
Shakila
Amri Nyani aliyejishindia kitita cha shilingi Milioni 140 huku
'akimbust' Mama yake kwenye sehemu ya usindi wake kwa kumpa kiasi cha
shilingi milioni 30.

Mchezo
wa namba unaongoza nchini Tanzania wa Tatu Mzuka leo umemtangaza na
kumtambulisha mbele ya vyombo vya habari mama aliyejinyakulia kitita cha
milioni 140 na wakati huo ‘kumbusti’ mama yake kwenye sehemu ya
ushindi wake.

Shakila Amri Nyani, ambaye ni mkazi wa Newala,
Mtwara na mama wa watoto 3 alisherehekea siku ya mama duniani kwa kumpa
mama yake milioni 30 kama ishara ya kutambua mchango wake katika siku
hiyo muhimu.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TatuMzuka, Bwana Sebastian Maganga alikuwepo kuwakab
idhi hundi Bi Nyani pamoja na mama yake. “Mama zetu ni hazina na hakuna kiwango chochote cha pesa kinachoweza kutosha kulipa upendo, msaada na kazi kubwa walioifanya katika kutulea. Kwa ushindi huu Tatu Mzuka tunaamini Bi Nyani na mama yake watafurahia na kuboresha maisha yao pamoja na familia zao” alisema Maganga

Bi Nyani, mwenye miaka 38 alikuwepo kuelezea furaha yake na namna ambavyo alicheza mpaka akapata ushindi huo mnono wa milioni 140.“ Nimekuwa nikicheza Tatu Mzuka kwa muda mrefu sasa. Nina furaha kubwa sana. Sikuwahi hata kuota kama naweza kupata nafasi kama hii. Mimi ni mjasiriamali na ninapanga kutumia pesa nilizoshinda kuongeza mtaji wa biashara yangu” alisema Bi Nyani

Bi Fatuma Bakari ambaye ni mama mzazi wa Nyani aliishukuru Tatu Mzuka kwa kuja na kampeni ya ‘Wiki Maalumu ya mama’ ambayo imemfanya akabustiwa kwa pesa nyingi baada ya mtoto wake kushinda.“Mimi pia nitatumia pesa nilizobustiwa kuwabusti ndugu wengine na kufanya shughuli za maendeleo ili kuboresha hali ya maisha ya familia yangu.” Alisema Bi Fatuma

Maganga alimalizia shughuli kwa kutoa dondoo ya kampeni mpya ilioanza leo – Mzukapaswedi. “Na hapa kinachohitajika ni namba zako 3 tu!! Za Bahati, ambazo zitakufanya ufikie mafanikio yako,iwe ni kuongeza elimu,kununua gari,kujenga frame za maduka, kuwekeza kwenye kilimo, nk, fanikisha matunda ya mzuka-paswedi yako kwa ushindi wa laki 1 hadi millioni 6 kila saa.
Ushindi wa millioni 10 katika mzuka deile leo saa tatu na nusu usiku, na ushindi wa millioni 60, jumapili hii kuanzia saa 3 na nusu usiku, tuma 500 hadi 30,000 kwenda namba ya kampuni 555111, na kumbukumbu namba ni namba zako 3 za bahati zikifuatiwa na neno mzukapaswedi kutoka 3mzuka, ukishinda Tanzania inashinda...

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)