Pichani kulia ni Muendesha boda boda Magembe Daniel akiwa na Mama yake Mzazi Mama Magembe,wakiwa wameshika mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 140 baada ya kuibuka mshindi wa mchezo wa kubahatisha TatuMzuka hivi karibuni
Magembe ambaye ni Mkazi wa Kibiti-Rufiji anamshukuru Mama yake Mzazi kwa kumlea vizuri,kama vile haitoshi anamshukuru zaidi kwa kumnunulia Piki piki na kuifanyia biashara,anasema na ndi maana mara baada ya kupata taarifa kuwa nimeshinda mchezo wa TatuMzuka,Mtu kwanza kabisa kumtaarifu alikuwa ni mama yake mzazi, kuwa ameshinda mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka,anasema mama yake hakuamini lakini alimtia moyo yakuwa na subira zaidi ili kubaini kama ni kweli ama la.
"Vijana wenzangu ninaofanya nao kazi wamenisihi nitulie,kwa sababu mara nyingi baada ya kuipata fedha nyingi, vijana hukengeuka,nilijiwekea nadhiri kuwa nikipata fedha nyingi ntafanya biashara zangu,lakini ndoto yangu kubwa ni kujenga nyumba kubwa ambayo ntaishi na familia yangu,ingawaje bado sijaoa",aliongeza kusema Magembe.
Pichani kulia ni Afisa Mkuu wa Masoko-Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha kijana mwendesha boda boda,Mageme Daniel aliyejinyakulia kitita cha shilingi milioni 140 za TatuMzuka hivi karibuni jijini Dar
Maganga alisema kuwa mpaka sasa mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka umevunja historia kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 20 za Kitanzania,ambazo zimekwenda kwa Washindi mbalimbali wa Mzuka Jackpot,Washindi wa Mzuka Daily na washindi mbalimbali,ambapo washindi milioni 58 wamejitokeza kujishindia mamilioni ya TatuMzuka.
"Tatumzuka imeendelea kuwa fahari ya wachezaji wa mchezo wa kubahatisha kwa sababu ina uwezo wa kutoa washindi wengi,hivyo nawaomba Watanzania waendelee kucheza mchezo huu,na kwamba hamasa kubwa ni kuendelea kuwafikia washiriki wengi zaidi kila kona ya nchi yetu,kuhakikisha mchezo huu unakuwa fahari ya Watanzania,wenye kuwaletea tija ya kimaendeleo katika nyanja mbalimbali",alisema Maganga.
Pichani kushoto ni Afisa Mkuu wa Masoko-Tatu Mzuka Sebastian Maganga akiwa pamoja na kijana mwendesha boda boda,Magembe Daniel aliyejinyakulia kitita cha shilingi milioni 140 za TatuMzuka hivi karibuni jijini Dar.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)