Airtel yazindua duka la kisasa Babati - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Airtel yazindua duka la kisasa Babati

 Babati District Commissioner Raymond Mushi speaks after launching a new Airtel Shop in Babati town yesterday.
Babati District Commissioner Raymond Mushi cuts a ribbon to officially launch a new Airtel Shop in Babati yesterday. He is flanked by Airtel Manager Manyara Region Polas Emmanuel

Mkuu wa wilaya ya BABATI mkoani MANYARA,RAYMOND MUSHI amewataka wakazi wa wilaya hiyo, kutumia fursa za mitandao ya simu kutunza fedha zao wanazopata baada ya kuuza mazao yao kwani itakalowasaidia kurahisisha biashara zao pamoja na kuepuka uwezekano wa kuporwa fedha za mauzo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la kampuni ya simu za mikononi ya AIRTEL wilayani BABATI,MUSHI amesema wakulima wengi wanatoka katika maeneo ya Vijijini hivyo wanashindwa kuhifadhi fedha zao sehemu salama lakini iwapo wakitumia vema duka hilo watawaweza kutunza fedha kwa urahisi na kufikia malengo waliyokusudia.
Naomba kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kujali wateja wao kwa kufungua duka hili la kisasa hapa. Ni nyinyi sasa mnaotakiwa kutumia huduma za Airtel kama Airtel Money ili kutunza fedha zenu. Nimepata taarifa kuwa kwa kutumia Airtel Money unaweza kutuma na kupokea fedha kutoka mtandao wowote hapa nchini, ukaifadhi fedha zako kwenye akaunti ya Airtel Money. Hii ni jambo njema na nawaomba mtumie hiyo nafasi kutumia huduma zao, alisema Mushi.
Meneja wa AIRTEL mkoa wa MANYARA, POLAS EMMANUEL amesema kampuni ya AIRTEL imelenga kuwawezesha wananchi kwakufikasha huduma vijijini.
Kufunguliwa kwa duka hilo ni mwendelezo wa kampuni ya Airtel kusogeza huduma karibu kwa wateja badala ya kuzifuata kwenye maduka makubwa mijini alisema Emmanuel huku akiongeza kuwa duka hili la kisasa ni moja ya maduka mengi katika kanda ya Kazikazini na  litatoa huduma zote zinazopatikana kwenye maduka makubwa,na hakuna kuwa na upungufu wa kutoa fedha, alisema Mushi
Kwa upande wake msimamizi wa duka hilo RICHARD MINJA amesema fursa hiyo ni muhimu kwani vijana wengi watapata ajira kutokana na huduma zitakazokuwa zinatolewa.
Mmoja wa watumiaji wa huduma ya AITEL, JOHN MMARI amesema kufunguliwa kwa duka hilo kutawasaidia kupata huduma za haraka hususani wanapotaka kutoa fedha na kuweka.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages