Pages

MSANII DIAMOND KUTOA BURUDANI KOMBE LA DUNIA 2018 NCHINI URUSI

 Msanii Diamond akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es alaam (katikati) ni Sealouise Shayo, Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini (kulia) ni Meneja wake Sallam SK.
 Msanii Diamond na Nahreel katika mkutano wa waandishi wa habari, wengine ni maofisa wa Coca-Cola na mameneja wa msanii Diamond.
Maofisa wa Coca-Cola wakiwa katika picha ya pamoja na Diamond na Nahreel baada ya mkutano na waandishi wa habari.

Msanii nguli wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz, kwa kushirikiana na kampuni ya Coca-Cola ametangaza kuwa ameshiriki kuimba wimbo utakaosherehesha Kombe la Dunia 2018 uitwao Colours.

Wimbo huo uliotungwa na mwanamuziki Jason Derulo wa Florida, Marekani, Diamond ameshiriki kuweka maudhui ya lugha ya Kiswahili na umetayarishwa na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na maprodyuza kutoka nchi nyingine chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema anayo furaha kupata fursa ya kushiriki kuimba kuimba wimbo wa mashindano haya makubwa ya kidunia na kuitangaza Tanzania na lugha ya Afrika bila kusahau tasnia ya muziki kwa ujumla.

“Kwangu hii ni nafasi nyingine ambayo najivunia kuipata ya kutangaza muziki wa kitanzania sambamba na lugha ya Kiswahili kwa kuwa sehemu niliyoshiriki kuimba nimetumia lugha ya taifa la Tanzania ambayo inazidi kupata umaarufu mkubwa duniani”alisema Diamond

Kwa upande wake Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo, alisema kampuni ya Coca-Cola ambayo ni moja ya mdhamini wa mashindano haya makubwa ya soka duniani inayo furaha kwa msanii kutoka nchini Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano haya. “Tuna imani watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya mashindano haya”alisisitiza.

Prodyuza nguli wa muziki nchini na kanda ya Afrika Mashariki, Nahreel ,ambaye ameshiriki kutengeneza wimbo huu aliishukuru kampuni ya Coca-Cola kwa jitihada mbalimali ambazo imekuwa ikifanya kuwanyanyua wasanii wa hapa nchini ambapo mbali na Diamond naye ameshiriki kwenye tukio hili kubwa. “Ninayo furaha ya kufanya kazi na Diamond kwa mara nyingine katika tukio hili kubwa la mashindano ya Kombe la Dunia na najivunia heshima kubwa tuliyopewa”

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)