Pages

MAFUNDI MITAMBO REDIO 25 ZA KIJAMII WATEMBELEA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC KUJIFUNZA KWA VITENDO

Principle Engener kutoka TBC, Noel Mtenga akitoa ufafanuzi kuhusu gari la kurushia matangazo la TBC 1 linavyofanya kazi wakati wa mafunzo kwa vitendo kwa mafundi mitambo kutoka redio jamii 25 zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar.
Mwahariri wa Habari za Kimataifa wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Nyambona Masamba akiwaelezea mafundi mitambo wa Radio za jamii kuhusu namna wanavyopata habari za Kimataifa pamoja na jinsi wanavyozihariri kabla ya kurushwa hewani wakati wa ziara ya mafunzo yaliyofanyika katika Shirika la Utangazaji(TBC).
Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Ramadhan Mpenda akiwaelezea kiwaelezea mafundi mitambo wa Radio za jamii namna wanavyorusha habari kwenye moja ya studio ya TBC 1 iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Fundi mitambo wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Fanuel Elia akitoa ufafanuzi kuhusu namna wanavoweza kupangilia vipindi kwenye chumba cha kusimamia matangazo ya TBC 1 wakati wa ziara ya mafunzo kwa mafundi mitambo wa Radio za jamii.

MAFUNDI mitambo wa redio kutoka mikoa mbalimbali nchini wametembelea Shirika la Utangzaji Tanzania(TBC)kwa lengo la kupata mafunzo zaidi ili kuendelea kuboresha majukum yao kwa ufasaha.

Wakiwa TBC mafundi mitambo hao wamepata nafasi ya kutembelea vitengo mbalimbali ambavyo vinahusika na masuala ya utangazaji katika shirika hilo.

Mafundi mitambo hao wametembelea TBC jana jijini Dar es Salaam na hatua hiyo ni muendelezo wa mafunzo yanayoendelea kutolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), ambalo limeamua kuwapiga msasa mafundi mitambo kutoka redio 25 za kijamii Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa mujibu wa Unesco ni kwamba mafundi mitambo hao licha ya kuata mafunzo kwa kukaa darasani, watapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo na kwenda kwao TBS ni sehemu ya kuendelea kuwajengea uwezo. Mafunzo ambayo ni sa siku saba yanatarajia kumalizika Aprili 25 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)