Pages

KUMBUKUMBU YA MIAKA 22 YA KIFO CHA DR. FRANCIS MW. MSELLEMU

DR. FRANCIS MW. MSELLEMU
1941- 1996

Baba, Ni Miaka 22 sasa tangu uondoke hata bila ya kutuambia neno la KWAHERI!

Maisha yetu hayajawahi kuwa rahisi bila uwepo wako, Baba.

Japo watu wanatuona tukicheka , hawajui ni kiasi gani mioyo yetu inahuzunika kwa kukukosa malezi, mapenzi na uwepo wako wewe.

Hata hivyo tunamshukuru MUNGU kwa kuendelea kutulinda, kututunza na kutubariki. Ameedelea kuwa kweli kwetu Mume wa Mjane na Baba wa Yatima.

Tunakuombea Pumziko la Milele, na tukiamini kwamba siku moja tutakutana na tutaimba Halleluya pamoja na wewe mbinguni.

Unakumbukwa daima na Mke wako Mpendwa Kodawa Mikaline Msellemu - ‘Mama K’ kama ulivyo kuwa umezoea kumuita, Watoto, Wakwe zako, pamoja na Wajukuu. Ndugu , Jamaa na Marafiki nao hawajakusahau.

‘Mamillioni Wanaitegemea’-Pumzika kwa Amani DAD!

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)