Pages

KATIBU MKUU WA CCM KOMREDI KINANA AWAASA WANA CCM KUMUUNGA MKONO MWENYEKITI WAO,RAIS DKT MAGUFULI KATIKA VITA YA KUPAMBANA NA RUSHWA PAMOJA UFISADI

 Katibu MKuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mjumbe wa kamati kuu ya siasa ya Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema Nchimbi jana mara baada ya kuwasili katika Kata ya Ilongero,Singida vijijini katika jimbo la Singida la Kaskazini,ambapo Chama cha Mapinduzi jana kilikuwa kinapiga kura za maoni kumchagu Mbunge atakaekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA.
 Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Singida Vijijini wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahamani Kinana alipokuwa akizungumza nao kabla ya kupiga kura ya kumchagua atakaewawakilisha katika nafasi ya Ubunge,na hatimaye kugombea katika uchaguzi mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika jimboni humo hivi karibuni.
Mjumbe wa kamati kuu ya siasa ya Mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt Rehema
Nchimbi akizungumza mapema jana kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya uliokuwa ukifanyika jana katika kata ya Ilongero,Singida
vijijini katika jimbo la Singida la Kaskazini,ambapo Chama cha Mapinduzi
kinamtafuta Mbunge atakaekiwakilisha
chama hicho katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi
karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo
hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA. 
 Katibu MKuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mapema jana kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya uliokuwa ukifanyika jana katika kata ya Ilongero,Singida
vijijini katika jimbo la Singida Kaskazini,ambapo Chama cha Mapinduzi
kilikuwa kikipiga kura kutafuta Mbunge atakaekiwakilisha
chama hicho katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi
karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo
hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA.Ndugu Kinana aliwaasa Wajumbe hao kumchagua mtua anaefaa na atakawasaidia na kuwasemea matatizo yao,na atakae kuwa tayari kuwaletea maendeleo.
Wajumbe wakimsikiliza Ndugu Kinana kwa umakini kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wananchi waliovutiwa na hotuba ya Katibu Mkuu Ndugu Kinana,ilibidi wasogee zaidi na kuendelea kusikiliza

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida Ndugu Juma Kilimba akimkaribisha Mgeni rasmi,Katiibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliyepita kuwasalimia na kuona wamejiandaaje na uchaguzi wao wa kura za maoni kwa ajili ya kumchagu Mtu atakaewawakilisha katika uchaguzi Mdogo wa Ubunge unaotarajiwa kufanyika hivi
karibuni,kufuatia jimbo hilo kuachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo
hilo Mh.Lazaro Nyalandu aliyehamia CHADEMA.Ndugu Kinana aliwaasa Wajumbe
hao kumchagua mtua anaefaa na atakawasaidia na kuwasemea matatizo
yao,na atakae kuwa tayari kuwaletea maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)