Pages

UMOJA WA MATAIFA WAZINDUA OFISI KATIKA MAKAO MAKUU YA NCHI, DODOMA

Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umezindua rasmi ofisi zake mjini Dodoma ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhamisha makao yake makuu. Ofisi hiyo, iliyo katika Mtaa wa Mlimwa, Area D, itakuwa na ofisi za mashirika 7 kati ya 23 ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi nchini Tanzania hivi sasa. Mashirika hayo saba yatakayotumia ofisi hizo ni pamoja na UNICEF, UNDP, UNFPA, UN Women, IOM, FAO na WHO.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa Kassim, ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, ambapo ofisi hizo sasa ni rasmi kuendesha shughuli za Umoja wa Mataifa kutokea mkoani Dodoma. Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith S. Mahenge, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro Rodriguez; Mwakilishi wa Nchi wa UNICEF, Bi.Maniza Zaman, wafanyakazi wa UN, maofisa wa Serikali na wanafunzi walioalikwa kutoka shule mbalimbali za mkoani Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini eneo la Mlimwa mjini Dodoma, Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustinew Mahiga na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Akizungumza wakati wa tukio hilo; Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Rodgriguez, alisema, “Uzinduzi wa ofisi hii utawezesha na kukuza ushirikiano wa Umoja wa Mataifa na Serikali hasa katika kipindi hiki muhimu Serikali inapohamia Dodoma.
Umoja wa Mataifa hufanyakazi kwa karibu na Serikali, na ofisi hii ni hatua ya kwanza katika Umoja wa Mataifa kuhamia Dodoma.”
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustine Mahiga akizungumza katika ufunguzi wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi w UNDP Nchini uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Akitoa shukrani zake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Maniza Zaman, alisema mashirika ya Umoja wa Mataifa hushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuunga mkono mpango wake wa maendeleo wa miaka mitano kupitia Mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP II).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akizungumza katika ufunguzi wa Ofisi yake uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP. nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez na wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustine Mahiga (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Wapili kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez na wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dr. Augustine Mahiga (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Waziri Mkuu,. Kassim Majaliwa akifungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata keki ikiwa ni moja ya shughuli za ufunguzi wa ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mahariki, Dr. Augustine Mahiga. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma baada ya kufungua Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini , eneo la Mlimwa mjini Dodoma Desemba 7, 2017. Watatu kushoto waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mshariki, Balozi Dr. Augustine Mahiga na watatu kulia waliokaa ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Matifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. Alvaro Rodriguez. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkluu)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)