Pages

DC MCHEMBE AZINDUA KAMPENI YA KUPANDA MITI WILAYA YA GAIRO KATA KWA KATA

 Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akizungumza machache na wananchi waliofika katika uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akipanda miti kuashiria uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe akielekea eneo la tukio na wananchi eneo la tukio.

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shaidi Mchembe amezindua kampeni ya kupanda miti Kata kwa Kata.

Akizungumza jana wakati akizindua kampeni hiyo iliyofanyika katika tarafa la Nongwe kata ya Chanjale, alisema kuwa wananchi ni lazima waheshimu kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti na si kuikata ovyo.

Katika kampeni hiyo Mhe. Siriel aliambatana na Meneja wa Misitu Wilaya Bw. David Maiba waliweza kuwahamasisha wananchi kupenda mazingira maana ndiyo yamekuwa yakisababisha wao kupata nvua.

"Nawaomba wananchi mpende kuhifadhi mazingira maana ndiyo uhai wetu ambao unasababisdha hata mvua kupatikana, sehemu ikiwa jangwa hamuwezi pata hata maji, niwaombe sana mtunze mazingira kwa ukaribu sana," alisema mhe. Siriel.

Kampeni hiyo imeanzia Tarafa ya Nongwe Kata ya Chanjale. Tarafa hii ipo uwanda wa juu ambapo mvua tayari zimeanza.

Viongozi wengine ambao aliambatana nao ni Diwani wa Chanjale Mhe. Maswaga Malima, Mtendaji Kata Bi. Stella Ngomano, Wenyeviti wa Vijiji, Watendaji wa Kata, Wazee Maarufu, Viingozi wa Dini na wananchi kwa ujumla.

Kata ya Chanjale ina Misitu ya Hifadhi yenye ukubwa wa ekari 3,000.

Aliongeza kuwa upandaji wa miti utakuwa ni zoezi endelevu na ameshaagiza kila kijiji kiwe na kitalu cha kuzalisha miti japo changamoto inayowakabili ni viriba, ambapo wanahitaji viriba zaidi ya milioni moja kwa Wilaya yote ya Gairo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)