Tarehe 25 mwezi wa tisa msanii wetu wa Pangani Bi Flora Nicholas Mdahila ambaye aliigiza kwenye filamu ya AISHA kama Miriam, mdogo wake wa AISHA aliteuliwa kwa ajili ya TUZO inayoitwa SOTIGUI AWARD, huko Ouagadougou nchi ya Burkina Faso.
Flora ni mwenyeji wa Kijiji cha Msaraza, kata ya Bushiri. Kuigiza kwenye filamu ilikuwa ndoto yake tangu alipokuwa mtoto. Kabla ya kuchaguliwa kushiriki kwenye
filamu ya AISHA, Flora alicheza kwenye vikundi mbali mbali vya sanaa hapa Pangani kwa ajili ya kuboresha kipaji chake. Juhudi zake hazikuwa bure. Wataalamu wa filamu walikiona kipaji chake. Kwa hiyo aliteuliwa kwa ajili ya kundi la Tuzo ya Sotigui ya Mashariki ya Afrika. Lengo la tuzo hii ni kutangaza na kukuza vipaji vya wasanii wa Kiafrika duniani. Filamu ya AISHA ilitengenezwa mwaka
2015 wilayani Pangani kama sehemu ya mradi wa mawasiliano ya shirika la UZIKWASA.
Ni filamu ya Wanapangani na wasanii zaidi ya asimilia 90 walioigiza kwenye Filamu ni wenyeji wa Pangani. Filamu hii ilipata sifa kubwa hapa Tanzania na dunia nzima. Ilifanikiwa kupata tuzo mbali mbali ya kimataifa huko Marekani, Ulaya na nchi mbali mbali za kiafrika.
Sasa ni zamu ya Flora kupata tuzo. Tutaendelea kuwataarifu kuhusu yatakayotokea. Sisi UZIKWASA tunasikia fahari sana na tunampongeza Flora kwa mafanikio haya makubwa. Habari kwa Hisani ya Anko Moo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)