TANAPA YAMTUNUKU TUZO MWASISI WA KITUO CHA UTAFITI MASOKWE, JANE GOODALL - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TANAPA YAMTUNUKU TUZO MWASISI WA KITUO CHA UTAFITI MASOKWE, JANE GOODALL

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, akimkabidhi Tuzo ya Uhifadhi Wanyama aina ya Sokwe, Dkt. Jane Goodall, aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama hao kwa miaka 60 katika Hifadhi ya Gombe.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, akimkabidhi Tuzo ya Uhifadhi Wanyama aina ya Sokwe, Dkt. Jane Goodall, aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama hao kwa miaka 60 katika hifadhi mbalimbali na baadaye kujikita katika Hifadhi ya Gombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, George Waitara. 

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, amemtunuku Mwanasayansi na Mtafiti wa Kimataifa wa Wanyama aina ya Sokwe, Dk Jane Goodall, tuzo maalumu ya kutambua mchango wake katika kuwatunza sokwe kwenye hifadhi ya taifa ya Gombe.
Kwa niaba ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dk. Jane  pia amekabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwamo cheti cha kutambua mchango wake, sanamu ya sokwe pamoja na picha ya sokwe.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Profesa Maghembe alisema Dk. Jane ametoa mchango mkubwa kwenye sekta ya uhifadhi kwa kubainisha tabia za sokwe ambazo watu wengi hawazijui.
Profesa Maghembe alisema mtafiti huyo ambaye ni raia wa Uingereza amebainisha katika tafiti zake kwamba sokwe wana fikiri na wana hisia kama walivyo binadamu.
Kutokana na hali hiyo, aliwata taasisi ya Jane Goodall ambayo inafanya tafiti mbalimbali za wanyama kufundisha Watanzania hapa nchini ili waendeleze kazi kubwa aliyokuwa akiifanya. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


"Dk. Jane amejenga timu ya watafiti na anatambulika duniani kote. Serikali pia tunatambua mchango wake katika uhifadhi wa sokwe, kazi ambayo ameifanya kwa muda mrefu," alisema Profesa Maghembe.
Naye, Dk. Jane amefurahishwa na hatua iliyofikiwa na TANAPA ya kutambua mchango wake katika utunzaji wa sokwe, jambo ambalo limempa nguvu ya kuendelea na kazi hiyo.
Alisema tangu akiwa mdogo alikuwa  anapenda sana wanyama na ndoto yake kubwa ilikuwa kuja Afrika kuangalia wanyama ambapo aliitimiza mwaka 1960.
"Nikiwa msichana mdogo, wenzangu walinicheka nilipowaambia nataka kwenda Afrika. Lakini nilipokuja na kwenda kuwasimulia kuhusu sokwe walifurahi na kuja kutembelea hifadhi mbalimbali za Tanzania," alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allen Kijazi alisema Dk. Jane alitumia miaka 57 kuhakikisha anafanya utafiti wa kutosha.
Kijazi alisema pia mtafiti huyo aliipa TANAPA taarifa mbalimbali kuhusu mwenendo wa sokwe jambo limeisaidia mamlaka hiyo kujia idadi ya wanyama hao.
"Asingetupa taarifa hizo huenda idadi ya wanyama hao ingepungua bila sisi kujua,"alisema.
 Akikabdhiwa Cheti cha kutambua mchango wake katika uhifadhi
 Dkt. Goodall, akifurahia cheti chake baada ya kukabidhiwa.
 Akikabidhiwa zawadi
 Akizungumza katika hafla hiyo....wakati akifafanua kuhusu utafiti wake katika kipindi chote toka alipoanza utafiti. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, George Waitara, akizungumza wakati wa Hafla hiyo.
 Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.
 Wakifurahia hotuba....
 Baadhi ya Wajumbe wa Bodi
 Baadhi ya wageni wakitembelea kujionea baadhi ya picha za Sokwe katika hafla hiyo.
 Baadhi ya wageni wakipata maelezo kuhusu maisha ya Sokwe
 Wasanii wanaounda bendi ya Spanest inayomilikiwa na TANAPA, wakipiga picha ya kumbukumbu na Mtafiti Mkuu wa Hifadhi ya Gombe, Dkt. Anthony Corins (wa tatu kushoto).
 Dkt. Jane Goodall, akieleza jambo kwa Wajumbe wa TANAPA, James Lembeli (kushoto) na Prof. Wineaster Anderson, wakati wa hafla hiyo.
 Mtafiti Mkuu wa Hifadhi ya Gombe, Dkt. Anthony Corins, akitoa maelezo kwa Waziri Maghembe, alipotembelea chumba cha maonyesho ya Picha za Sokwe katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allen Kijazi, akizungumza katika hafla hiyo.

 Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Sarah Cook, akizungumza katika hafla hiyo 
 Wasanii wa Bendi ya Spanest wakitoa burudani katika hafla hiyo. 
Picha za pamoja baada ya hafla hiyo,

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages