MAAJABU: SIMBA AKUTWA AKIMNYONYESHA MTOTO CHUI TANZANIA!! - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAAJABU: SIMBA AKUTWA AKIMNYONYESHA MTOTO CHUI TANZANIA!!

Tanzania inaingia tena kwenye vitabu vya historia na maajabu, baada ya kwenye moja ya mbuga kupatikana Simba akimyonyesha mwana wa chui.

Wawili hao walionekana na Joop Van Der Linde mgeni katika katika eneo la Ndutu safari Lodge hapa nchini katika eneo la uhifadhi la wanyama pori la Ngorongoro.

Limekuwa tukio la ajabu kwa sababu ya utofauti wa jamii ya wanyama hawa, Simba akitokea jamii ya Leo na Chui akitokea jamii ya Tigris. Wote wakiwa ni Panthera.

Eneo hilo ni la Serengeti. Simba huyo amepewa jina Nosikitok na ana umri wa miaka mitano.
Simba huyo amewekewa mfumo wa GPS katika shingo yake ili kutambua anakokwenda na ana watoto watatu waliozaliwa kati ya mwezi Juni 27-28.

Chanzo cha habari: BBC SWAHILI
Picha na Joop Van Der Linde/ Ndutu safari Lodge

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages