Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imepongeza juhudi za Taasisi ya Kijamii ya Tulia Trust kwa kuwezesha kusomesha vijana 20 masomo ya Sanaa na Utamaduni katika taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) huku akiziomba wadau wengine kuiga mfano huo.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya masomo kwa vijana hao 20 waliodhaminiwa na Tulia Trust, Kaim Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bi. Leah Kilimbi,ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Wizara hiyo,amewataka vijana hao kuwa Mabalozi wazuri ili wakawafundishe na wengine kile walichojifunza hapo.
“Sisi kama Serikali. Tunafarijika sana kwa namna wadau wanavyosaidiana nasi katika kuleta maendeleo katika Nyanja mbalimbali. Taasisi ya Tulia Trust imeonyesha nia na tunaipongeza sana kwani imesaidia vijana wetu kujifunza Sanaa, Utamaduni na kila aina ya mafunzo. Tunaamini huko waendako watakuwa mabalozi wazuri sana pia wadau wengine waige mfano huu” alieleza Bi. Leah Kilimbi.
Kwa upande wao Mabalozi wa Tulia Trust, akiwemo Hassan Ngoma aliweza kuwa taasisi hiyo itaendelea kusaidia jamii ya Watanzania wote na mipango yao kusaidia katika Nyanja mbalimbali huku kupitia Sanaa wameweza kuwasomesha Vijana hao ambao wametokana na tamasha linaloandaliwa kila mwaka na taasisi hiyo.
Naye Balozi wa Tulia Trust,Msanii Ditto alieleza kuwa, vijana hao kwa sasa wanatakiwa kuwa kioo kwa jamii na walichojifunza hapo watakuwa walimu wa wengine huku akibainisha kuwa kwa sasa baadhi ya nyimbo zake zinanafasi kubwa ya kuingiza ala za asili ikiwemo midundo.
Nao baadhi ya vijana hao waliishukuru Tulia Trust kwa ufadhili huo na kuahidi watafanyia kazi kila walichojifunza.
Mafunzo hayo maalumu ya Sanaa na Utamaduni kwa vijana hao kutoka wilaya za Rungwe, Busokelo na Kyela, Mkoa wa Mbeya yalioendeshwa na TaSUBa kwa kushirikiana na Tulia Trust na yaliendeshwa kwa muda wa miezi miwili.
Aidha, vijana hao waliweza kufanya onyesho maalumu katika ukumbi wa Chuo hicho ambapo pia walitunukiwa vyeti na mgeni rasmi, Bi. Leah Kilimbi.
Mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha vijana hao kufanya shughuli zao za ngoma za asili kiutalaamu zaidi, hali itakayowaongezea kipato na kuwafungulia fursa nyingi zaidi.
Vijana hawa wametoka kwenye vikundi vya ngoma ambavyo vilivyoshiriki tamasha la Ngoma za Asili la Tulia linalofanyika kila mwaka.
Hii ni awamu ya kwanza ya ufadhili wa Taasisi ya Tulia trust, awamu ya pili inayofuata itanza katika katika mwaka wa masomo 2017/2018 ambapo itahusisha vijana 7 ambao watapata mafunzo katika ngazi ya Stashahada (Diploma) na Astashahada (Certificate) katika fani za Sanaa za maonyesho na ufundi (performing and visual arts).
Kaimu Mtendaji Mkuu wa TaSUBa, Gabriel Kiiza akizungumza katika tukio hilo la ukabidhiwaji wa vyeti kwa vijana hao 20 waliofadhiliwa kwa msaad wa Tulia Trust. Tukio limefanyika chuoni hicho Juni 16.2017, Mjini Bagamoyo.
Balozi wa Tulia Trust Hassan Ngoma akizungumza katika tukio hilo la ukabidhiwaji wa vyeti kwa vijana hao 20 waliofadhiliwa kwa msaad wa Tulia Trust. Tukio limefanyika chuoni hicho Juni 16.2017, Mjini Bagamoyo.
Kaim Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bi. Leah Kilimbi akizungumza katika tukio hilo
Baadhi ya vijana hao wakiwa katika maonesho yao maalum ikiwemo ya upigaji wa ngoma na kucheza wakati wa kuhitimu mafunzo yao
Baadhi ya vijana hao wakiwa katika maonesho yao maalum ikiwemo ya upigaji wa ngoma na kucheza wakati wa kuhitimu mafunzo yao
Kaimu Mtendaji Mkuu wa TaSUBa, Gabriel Kiiza akizungumza katika tukio hilo la ukabidhiwaji wa vyeti kwa vijana hao 20 waliofadhiliwa kwa msaad wa Tulia Trust. Tukio limefanyika chuoni hicho Juni 16.2017, Mjini Bagamoyo.
Baadhi ya vijana hao wakiwa katika maonesho yao maalum ikiwemo ya upigaji wa ngoma na kucheza wakati wa kuhitimu mafunzo yao
Vijana hao wakikabidhi risala yao kwa uongozi wa Tulia Trust
Meza kuu ikifuatilia tukio hilo
Baadhi ya vijana hao wakiwa katika maonesho yao maalum ikiwemo ya upigaji wa ngoma na kucheza wakati wa kuhitimu mafunzo yao
Baadhi ya vijana hao wakiwa katika maonesho yao maalum ikiwemo ya upigaji wa ngoma na kucheza wakati wa kuhitimu mafunzo yao
Baadhi ya vijana hao wakiwa katika maonesho yao maalum ikiwemo ya upigaji wa ngoma na kucheza wakati wa kuhitimu mafunzo yao
Baadhi ya vijana hao wakiwa katika maonesho yao maalum ikiwemo ya upigaji wa ngoma na kucheza wakati wa kuhitimu mafunzo yao
Ditto akieleza machache katika tukio hilo
Kaim Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bi. Leah Kilimbi akizungumza katika tukio hilo
Kaim Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bi. Leah Kilimbi akiwa amepiga picha ya pamoja na Vijana hao 20 waliohitimu mafunzo hayo ya Sanaa. Tukio hilo limefanyika Juni 16.2017, Mjini Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)