TV 1 YAJITOSA KUTAFUTA FEDHA ZA MASHINDANO UA TENIS YATAYOFANYIKA MEI NCHINI ITALY - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TV 1 YAJITOSA KUTAFUTA FEDHA ZA MASHINDANO UA TENIS YATAYOFANYIKA MEI NCHINI ITALY

 Katibu mkuu wa Chama cha Tennisi nchini , Irene Jackson Mwasanga  akizungumza na waandsihi wa habari juu ya mpango wa kuiwezesha timu ya mchezo wa Tennisi kwa walemavu
 Meneja Masoko wa TV 1 Tanzania , Gllian Rugumamu akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpango wa T V 1 Kusaidia timu hiyo hili iweze kusafiri kwenda Italy kushiriki mashindano ya Dunia.
 Promotion Meneja wa kituo cha radio cha Times Fm, Namiundu Ngutupari  akizungumza juu ya kituo hicho kujiingiza katika kusaidia kupatikana kwa fedha za wachezaji hao kuwawezesha kufika nchini Italy katika mashindano ya Dunia
 Meneja Masoko wa kampuni ya bima ya Tanzania Management Insuarance ,Johnson  Wariko akizungumzia jinsi kampuni yake ilivyojipanaga kuwawekea bima wachezaji hao ambao watasafiri kwenda nchini Italay
Na Chalila Kibuda.

Timu ya Magongo ya Tennis inahitaji milioni 120 ili kuweza kushiriki mashindano ya kimataifa yanayotarajia kutimua vumbi Mei 1 hadi Mei 6 nchini Italy. Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Rais wa timu hiyo,  Denis Makoi amesema kuwa hadi sasa wamepata dola 3500 ambazo dola 3000  zimetolewa na  Kampuni ya TPS  na dola 1500 zimetolewa na shirikisho la Tenis la Kimataifa.

Amesema mashindano  hayo ni mhimu kwa timu hiyo kwani wao ndio

mabingwa wa Afrika hivyo kushiriki kwao kutaongeza kuwa na uwezo na kuiletea Taifa heshima ya mchezo huo. Makoi amesema kuwa TV One wamejitoa kuungana na katika kutafuta fedha hizo ili timu hiyo iweze kushiriki mashindano  hayo yatayoifanya Tanzania kuingia katika ramani mchezo wa Tenis.


Meneja wa Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu amesema wamejitoa katika kuhamasisha watanzania kuchangia timu hiyo ili iweze kushiriki mashindano hayo. Gillian amesema kama chombo cha habari wanawajibu wa kuhamasisha mchezo wa tenis kutokana na vjana kuwa na 
uwezo wa mchezo huo. 
Amewaomba watanzania kuchangia kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa M-Pesa kwa kuingiza namba 5590901 kwa Benki ya NIC kwa fedha ya Kitanzania  A/C No.2000021086 na dola za Kimarekani kwa akaunti  A/C NO. 2000021094.
 Mcheza Tenisi Vosta Piter akijaribu kurudisha mpira uliopigwa na mwenzie katika mazoezi ya mchezo huo katika Viwanja vya Gymkhana  Dar es Salaam
mcheza Tennisi akiwa katika mazoezi ya kawaida katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam leo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages