NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo Aprili 12, 2017 imekubali ombi la Wizara ya Sheria na Katiba, la kuruhusu Mtuhumiwa wa kusafirisha madawa ya kulevya, Ally Khatib Haji maarufu kama Shkuba, (pichani juu), na wenzake wawili Iddi Saleh Mfuru na Lwitiko Samson Adam, wasafirishwe kwenda Marekani kujibu mashtaka ya kusafirisha madawa ya kulevya.
Akitoa uamuzi huo leo, Hakimuwa Mahakama hiyo alsiema, anakubaliana na maombi ya serikali kama yalivyowasilishwa na vielelezo ikiwemo barua kutoka serikali ya Marekani ikiomba watuhumiwa hao kusafirishwa kwenda nchini humo kwani serikali ya Marekani ilikuwa inamsaka Shkuba kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa hakimu Cyprian Mkehe, watuhumiwa hao watasalia korokoroni wakisubiri serikali kutekeleza maombi yake ya kuwakabidhi watuhumiwa kwa serikali ya Marekani.
Hata hivyo Mahakama hiyo imetoa ruhusa ya siku 15 kuanzia siku ilipotoa uamuzi kwa upande wa watuhumiwa kukata rufaa Mahakama kuu kuomba watuhumiwa hao warejeshwe nchini ili waweze kuendelea na mashtaka yanayowakabili hapa hapa Tanzania.
Mwaka jana Marekani ilimtangaza Shkuba kuwa ni kinara wa usafirishaji wa madawa ya kulevya kwenye nchi za Afrika, Asia, Marekani ya Kaskazini kupitia Afrika Mashariki ambako ndiko kwenye “ngome” yake.
Shkuba alimatwa Februari 2014 akijiandaa kupanda ndege kwenda Afrika Kusini akiwa na kilo 210 za Heroin.
Shkuba akiwasili kwenye chumbacha mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo Aprili 12, 2017
Shkuba akiwasili kwenye chumbacha mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo Aprili 12, 2017
Shkuba, (katikati), akiwana watuhumiwa wenzake, Iddi Saleh Mfuru, (wapili kulia0 na Lwitiko Samson Adam,(wapili kushoto), wakiwa chini ya ulinzi wa askati Magereza ndani ya chumba cha mahakama
Lwitiko Samson Adam, akisindikizwa na askari magereza kuingia kwenye chumba cha mahakama
Ulinzi ukiwa umeimarishwa nje ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, wakati mahakama hiyio ikitoa uamuzi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)