Wafanyakazi wa Airtel kuitambulisha “Hatupimi Bando” Sokoni - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Wafanyakazi wa Airtel kuitambulisha “Hatupimi Bando” Sokoni

Meneja Uhusiano wa Airtel, Bwn Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari juu ya mpango wa Airtel kuitambulisha huduma ya Hatupimi Bando sokoni

Kufatia kuzinduliwa kwa ofa Kabambe ya Airtel ijulikanayo kama “Hatupimi Bando”  ofa inayowapa wateja wake uhuru wa kuongea bila kikomo, wafanyakazi wa Airtel wamejipanga kuingia sokoni na kukutana na wateja kwa lengo la kutoa elimu zaidi juu ya huduma na bidhaa za Airtel

Mpango huu unategemea kufanyaka leo ijumaa ambapo wafanyakazi wa Airtel nchi nzima watakutana na kuzungumza na wateja wao ana kwa ana katika maeneo mbalimbali na kuitambulisha ofa hii ya “Hatupimi Bando” pamoja na kuwaunga wateja wapya kwenye mtandao wa Airtel ili nao pia waweze kufurahia bidhaa na huduma mbalimbali na kujiunga na ofa hii kabambe ya “Hatupimi Bando”

“Tunapenda wateja wetu waelewe vyema ofa hii ya “Hatupimi Bando” itakayowasaidia kuokoa kiasi kikubwa cha gharama katika matumizi yao ya simu kwani ofa hii inawapatia gharama nafuu zaidi za mawasiliano  sokoni.

wateja wetu wanaweza kujinga “Hatupimi Bando” Kwa kiasi cha shilingi 1000/=  ,shilingi 5000 kwa wiki, na vilevile unaweza kujiunga na kwa mwezi kwa shilingi 10,000/= na kufurahia huduma yakutopimiwa dakika na kuongea bila kikomo”. Alisema Jackson Mmbando, Meneja Uhusiano wa Airtel

Kujiunga na ofa ya HATUPIMI Bando piga *149*99# kisha chagua 1 kupata HATUPIMI kisha chagua bando ya Siku, Wiki, Mwezi kulingana na mahitaji yako “ alisisitiza  Mmbando

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages