KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MRADI WA UMEME WA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MRADI WA UMEME WA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo, (aliyesimama), akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, wakati wa ziara ya kamati hiyo kutembelea Mradi wa Umeme wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam, leo Machi 23, 2017
Meneja Msimamizi wa Mradi wa Kinyerezi I, Yuka Mukaibo kutoka kampuni inayojenga mradi huo ya Sumitomo kutoka Japan, akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati walipotembelea eneo la Mradi jijini Dar es Salaam, Machi 23, 2017. Wakwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Palangyo, na wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.
 Naibu Mkurugenzi wa TANESCO, Mhandisi Khalid James, (aliyesimama), akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa Mradi huo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini waliotembelea kujionea maendeleo ya Mradi huo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages