Pichani ni Baadhi ya wakimbizi katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu wakipewa mafunzo toka kwa wafanyakazi wa Airtel huduma kwa wateja ya jinsi ya kutumia huduma ya Airtel Money tap tap card, kadi hiyo Inasaidia WFP kutuma Pesa kwa Wakimbizi katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu. Kadi ya Airtel Money Tap tap imeunganishwa na akaunti za Airtel Money ili kutoa usalama wa utumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya mtandao bila ya kuwa na simu ya mkononi.
· Kadi ya Airtel Money Tap Tap inatumiwa na wakimbizi katika manunuzi ya bidhaa na kutoa hela
· Huduma hii inatoa usalama wa utumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya mtandao bila ya kuwa na simu ya mkononi.
Airtel Tanzania imeanzisha njia mpya na rahisi ya Near – Field Communication (NFC) ambayo ni mfumo wa malipo utakaoisaida Shirika la chakula Duniani (WFP) kuhamisha fedha kwa wakimbizi wapatao 10,000 kama sehemu ya mgao wao wa chakula kwa miezi mitatu ikiwa ni mpango wa majaribio wa kuboresha huduma katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.
Chini ya majaribio hayo, kwa sasa wakimbizi hao watapokea fedha kwa njia ya simu ya mkononi yenye dhamani ya fedha za kimarekani $ 4.50 (shilingi 10,000) mara mbili kwa mwezi wakiwa katika kambi hiyo. Fedha hizo zitawekwa katika kadi zao za Airtel Money Tap Tap kadi zilizounganishwa na teknolojia ya malipo ya NFC ambao umeunganishwa na akaunti zao za Airtel Money. Tap Tap kadi inatoa urahisi wa malipo na ni njia rahisi inayomfanya mteja kufanya malipo bila ya kuwa na simu yake ya mkononi wakati wowote. Ni ufumbuzi mzuri kwa wakimbizi unaowawezesha kufanya shughuli za haraka na kwa urahisi kwa kugusisha tu kadi kadi zilizounganishwa na akaunti zao za Airtel Money na kufanya malipo ya kupokea au kununua bidhaa.
"Tap Tap kadi imeungwanishwa na huduma ya Airtel Money ili inatoa huduma ya kipekee na urahisi kwa wateja wetu katika utumiaji wa wa fedha kwa njia ya mtandao, inawawezesha wateja kutumia teknolojia ya kisasa kabisa yakufanya malipo au kuwa na uwezo wa kumiliki akaunti zao za fedha kwa njia ya mtandao hata kama simu ikiwa imezima," alisema Mkuu wa kitengo cha huduma cha Airtel Money, Isack Nchunda. "Tunafura kubwa kuona kadi hizi mpya zinawawezesha kufanya manunuzi ya chakula na kusaidia maisha ya wakimbizi waishio Tanzania."
Baada ya kupokea fedha kutoka kwenye kadi ya Tap Tap, wakimbizi wanauwezo wa kununua chakula katika soko la Nyarugusu ambalo lilifunguliwa mwaka 2016. soko, hilo lipo maeneo ya buffer zone kati ya kambi na wenyeji wa maeneo hayo, ambapo imewapa nafasi wafanyabiashara wa maeneo hayo kuweza kuuza mazao yao kwa wakimbizi.
"Matumizi ya kadi hizo inawarahisishia wakimbizi kukidhi mahitaji yao ya chakula na wakati huo huo kuinua uchumi wa nchi kwakuwa wanyeji hujipatia soko kwa bidhaa zao," alisema Mwakilishi wa WFP nchini Michael Dunford. "Pamoja na fursa kubwa ya kununua aina mbali mbali ya vyakula vinavyozalishwa ndani ya nchi na kuwasaidia kukidhi malazi, vilevile inasaidia kuboresha hali ya lishe ya kaya na kuhakikisha kwamba jamii na wenyeji pia wanafaidika kupitia shughuli nyingi za kiuchumi."
Katika kipindi hiki cha majaribio , wakimbizi wataendelea kupokea mafuta, uji na vitu vingine vidogo wakati mgawo wa wa nafaka, kunde na chumvi vitabadilishwa kwa fedha taslimu.alisisitiza Dunford
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)