Semina ikiendelea.
Meza kuu.
Mmoja wa maofisa wa Taasisi hiyo, Wilson Kibugu akitoa maelezo kwa wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina hiyo ya siku moja iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Wilaya hiyo.
Ofisa Utawala wa Taasisi hiyo, Fatma Shaib (kushoto),
akisoma lisala.
Mgeni rasmi Wanchoke Chinchibera akipokea lisala kutoka kwa Ofisa Utawala wa Taasisi hiyo, Fatma Shaib.
Mratibu Mradi wa Kilimo wa Taasisi ya Winamwnga Cultural Heritage Association, Saidi Simkonda (katikati), akitoa mada katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira yaliyofanyika wilayani Kisarawe mkoani Pwani juzi.
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Syngeta Tanzania Limited, John Ngoma akielezea ubora wa mbegu aina ya Sy 514 inayosambazwa na kampuni hiyo kupitia miradi ya kilimo ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Mradi wa kilimo wa Taasisi ya Winamwnga Cultural Heritage Association, Mwajuma Motto (katikati), akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani Kisarawe mkoani Pwani jana. Kulia ni Mwezeshaji, Filbert Luoga na kushoto ni mratibu wa miradi wa taasisi hiyo, Saidi Simkonda.
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot Mwasabwite akichangia jambo kwenye semina hiyo.
Dotto Mwaibale, Kisarawe
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani imetenga Kata 10 kwa ajili ya kilimo cha mkataba kitakachoendeshwa na Taasisi ya Winamwanga Cultural Heritage Association.
Mratibu wa mradi huo kutoka taasisi hiyo, Saidi Simkonda akizungumza juzi katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani humo juzi alisema mradi huo umelenga kuwainua kiuchumi wananchi wa Kisarawe na Mkoa wa Pwani kiujumla.
Alisema taasisi hiyo imepanga kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa ili kuinua uchumi wa wananchi kupitia vikundi vya ujasiriamali wa kilimo hai na ufugaji wa kuku chotara pamoja na kuwawezesha kupata fursa za mikopo katika asasi za kifedha zilizopo wilayani humo.
"Taasisi yetu imejipanga kuanzisha kilimo cha mkataba ambapo mazao yatakayopatikana itayanunua na tayari serikali ya Kijiji cha Kuluwi imetoa ghala la kuhifadhia mazao hayo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera alisema mradi huo utawasaidia wananchi na kuwa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imetenga kata kadhaa kwa ajili ya mradi huo ambazo ni Maluwi, Vikumburu, Kuluwi na Mafizi.
Alisema kwa sababu mradi huo ni mpya katika wilaya yao na utafanya shughuli zake kwa kilimo cha mkataba aliishauri taasisi hiyo kujenga ushirikiano mkubwa na wananchi kupitia vikundi ambavyo tayari vimesajili na majina yake kuwepo katika daftari ofisini kwa mkurugenzi wa halmshauri hiyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)