WATANZANIA SAIDIENI JAMII YA WATU WASIOJIWEZA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WATANZANIA SAIDIENI JAMII YA WATU WASIOJIWEZA

 Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea  bajeti mbalimbali  za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo

Na Woinde Shizza,Arusha.


Watanzania nchini wametakiwa kusaidia Jamii ya watu wasiojiweza ikiwemo walemavu,watoto yatima pamoja na wazee ili waweze kupata mahitaji yao na kuondokana na umasikini uliokithiri.




Hayo yameelezwa na Baadhi ya Wananchi waishio katika kata ya Kisongo mkoani Arusha ambapo walisema kuwa jamii ya wahitaji imekua ikiishi katika mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa anawasaidia jamii hiyo.

"katika jamii kuna watu wengi wakiwemo watoto wanatoto na watu wasio jiweza  ambao wanakaa katika mazingira magumu mno  hivyo ni wajibu wetu sisi  kuwasiaidia wale ambao awajiwezi ,mtu ukiwa na uwezao kidogo unatakiwa  ujijengee tabia ya kuwasiaida hawa wasio jiweza"alisema Sekela Tondolo



Kwa upande wake Mkazi mwingine wa kata ya  Kisongo Wiliam James Alisema kuwa  jamii ya wasiojiweza imekua ikisahaulika mara kwa mara hivyo ni jukumu la kila Mwananchi kuhakikisha kuwa anafanya kitu kwa ajili ya jamii yake kitakacholeta mchango ambao ni chanya na kuwawezesha kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo kimaisha.



Kwa upande wake Mheshimiwa Nabii Mkuu Dr. Geor  Davie  wa Huduma ya Ngurumo ya Upako  katika ibada ya makusanyo ya vitu na fedha kwa
ajili ya kuwasaidia wahitaji alisema kuwa taasisi za dini hazina budi kujikita
katika kuwasaidia wahitaji na wasiojiweza ili kuwa na taifa imara na endelevu .

"ni wajibu wa taasisi za kidini  ,makampuni mbalimbali , hata watu binafsi
ambao wanauwezo kuweza kusaidia watu hawa wenye mahitaji na walae wasio  jiweza ili nao wajisikie vyema na kuona nao  ni sehemu ya watu kama
wengine "alisema 
Geor  Davie



Huduma hiyo inautaratibu endelevu wa kila mwaka wa kupeleka mahitaji kwa wato wasiojiweza pamoja na kuwawezesha kiuchumi kaya zilizoathiriwa na umasikini kwa kiasi kikubwa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages