WALEMAVU WA KIJIJI CHA LULANZI WAMLILIA MBUNGE RITTA KABATI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WALEMAVU WA KIJIJI CHA LULANZI WAMLILIA MBUNGE RITTA KABATI


 Mbunge wa viti maalum mkoa waIringa(CCM) Rita Kabati akiongea na familia ya watu watano wenye ulemavu wa viungo alipowatembea katika kijiji cha Lulanzi kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa wakati wa kuwasaidia msaada kukarabati nyumba yao pamoja na kuwapa vitu vingine vya kimsaada

Leah mwamoto mtoto wa mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto naye alishuhudia maisha magumu wanaoishi familia ya watu watano wenye
ulemavu wa viungo alipowatembea katika kijiji cha Lulanzi kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa na hapo aliposimama ndio choo kinachotumiwa na familia hiyo kwa sasa huku wakisubili ujenzi wa choo kipya kinachoendelea kujengwa kwa hisani ya mbunge Ritta kabati

 Hivi ni baadhi ya vifaa vilivyoletwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati kwa ajili ya kuwasidia familia ya watu watano wenye wa viungo alipowatembea katika kijiji cha Lulanzi kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa

Na fredy mgunda,Iringa


FAMILIA ya watu watano wenye ulemavu wa viungo wamemuomba mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati kuendelea kuilea familia hiyo kama familia yake.


Akizungumza na blog hii 
mmoja wa wanafamilia hiyo,Elias Mpogole ambaye ni mlemavu alisema kuwa 
mbunge huyo amekuwa akiwasaidia toka siku ya kwanza walipokutana naye katika 
kijiji hicho cha Lulanzi.


“Zamani tulikuwa tunaishi 
kwenye nyumba ambayo inavuja haina dilisha wala mlango pia tulikuwa tunalala 
chini lakini mbunge Kabati katusaidia nyumba nzuri kama mnavyoiona waandishi, katuletea 
magodoro,mashuka,blanket na sasa ameanza kutujenga choo cha kisasa na 
ameshawalipa mafundi pesa zote ndio maana tunaomba anendelee kuwa na sisi.”Alisema 
Mpogole


Mpogole alishukuru msaada 
waliopatiwa na kuwataka wadau wengine waweze kujitokeza zaidi kuwasaidia 
kuwapatia vyakula na radio za kuwezakusikiliza nyimbo za dini.


Kwa upenda wake mbunge wa 
viti maalum mkoa waIringa(CCM) Rita Kabati ametoa msaada wa vitu mbalimbali 
ikiwemo ukarabati wanyumba kwa familia yenye watoto walemavu wanne wa kijiji 
cha Lulanzi kilichoko kata ya Mtitu wilayani Kilolo mkoa wa Iringa. 


Msaada huo wa ukarabati wa 
nyumba,umeambatana na magodoro, vyakula na ujenzi wa choo cha kisasa ameutoa 
baada yakuwahidi kufanyia matengenezo ya nyumba ambayo walikuwa wakipata shida 
kipindi cha masika mara baada ya kufanya ziara mapema mwaka huu katika kijiji
hicho nakugundua mateso wanayokumbana nayo familia hiyo. 


 "Nimeitembelea familia hiinimeumia sana 
kwani maisha wanayoishi ni ya shida sana hawana msaada wowotenyumba yao inavuja 
hawana chakula maishayao ni ya kuunganga unga mpaka watu  wajekama sisi kuwaletea vitu  vidogo vidogokama mchele na mafuta na mbaya Zaidi 
hata watoto hao wote watatu hakuna hatammoja aliyewahi kukanyaga shule ingawa
wanaonekana ni wakubwa hivyo jamii tunapaswa kuwasaidia watoto hawa” alisema Kabati  


Familia hiyo ambayo baba 
mzazi Mzee LucasMpogole mbaye kwa sasa amelazwa hospitali ya mkoa wa Iringa kwa 
ugonjwa wakupooza ina watoto wanne wote wakiwa walemavu wa viungo hivyo kukosa 
msaadakabisa pindi mvua zikianza kijiji hapo. 


Akizungumza wakati wa 
kukabidhimsaada huo , Kabati alisema kuwa jamii ya walemavu wanahitaji msaada 
wa hali namali kutoka kwa wadau wenye uwezo na kuacha tabia ya kuiacha serikali 
peke yakekatika kutatua kero zao na kuwahudumia.


Alisema kuwa msaada huo 
utawafarijiwalemavu hao waone kuwa pamoja na upungufu walionao bado jamii ya watanzaniainawathamini 
na kuwajali katika maisha yao ya kila siku.


 Aliongeza kuwa walemavu wanayo hakiya kuishi 
na kujitegemea iwapo jamii itawajengea uwezo badala ya kuwafungiandani na 
kuwaona kama ni mkosi katika familia ila kugundua vipajiwalivyonavyo na 
kuiwezesha serikali kuwaingiza katika mipango mbalimbali yakuwapatia huduma. 


Kabati alitoa wito kwa 
serikali kuona umuhimu wa kutumia vituo mbalimbali vinavyolea watoto wenye ulemavukuhakikisha
vinawejengea miundo mbinu rafiki na uboreshaji mipango na mfumo wautoaji elimu, 
afya na usafiri kulingana na tofauti za umri wa watoto nchini. Aidha Kabati alitoa 
wito kwa Mfukowa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuangalia kwa jicho la tatu familia 
ya Mpogolekwa kuwaongezea kipato zaidi cha kila mwezi kwani kwa hali waliyonayo 
na kiwango wanachopata kila baada ya miezi miwili hakiendani na uwingi wa 
walemavuwa familia hiyo maskini. 


Naye baba mdogo wa watoto hao 
akiongea kwa niaba ya baba mzazi wa walemavu hao, Juma Mpogole alimshukurumbunge 
huyo kwa msaada aliotoa na kumtaka awasomeshe watoto wake ambao tangu wazaliwe
hawajawahi pata elimu yoyote licha ya kufikisha umri wa miaka zaidi 20.


Lakini naomba nitoe rai kwa 
wale wanasiasa na wananchi wengine wanaokuja kupiga picha nah ii familia ya 
watu wenye ulemavu wa viungo kwa ajili ya kujitafutia umaarufu waache tabia 
hiyo.


“Kila mara tunaona waandishi 
na wapiga picha wanafika hapa na viongozi mbalimbali lakini kila siku wanatoa 
ahadi tu sioni msaada wowote ule unaotolewa zaidi ya kuona wanajitafutia 
umaarufu huko mitaani naomba waacha tabia hiyo sisi tunamuona mbunge Ritta 
Kabati na kaka yake mbunge wa jimbo hili la kilolo Vennence mwamoto ndio 
wanaosaidia familia hii,kweli familia hii inaitaji msaada hivyo njooni kutoa 
msaada sio kupiga picha pekee yake”.alisema Mpogole

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages