JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA LATOA TAARIFA YA USALAMA 2016 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA LATOA TAARIFA YA USALAMA 2016


Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo.Picha na Vero Ignatus Blog
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari leo 5Januari2017.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda Charles Mkumbo 5Januari
2017.

Pikipiki zilizokamatwa zikiwa zimepaki makao makuu ya polisi mkoa wa Arusha. 

Magari yaliyokamatwa kwa makosa mbalimbali yakiwa yamepakiwa makao makuu ya polisi mkoani Arusha
Baadhi ya magari yaliyopata ajali yakiwa

Baadhi ya Magari yaliyopata ajali na kukamatwa kwa makosa yakiwa yamepaki katika kituo kikuu cha polisi mkoani Arusha .Picha na Vero Blog


Na.Vero Ignatus ,Arusha.


Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limetoa taarifa juu ya usalama barabarani kuanzia Januari 2016 –Desemba  ,ambapo limesema kuwa takwimu za kiahalifu zimepungua kwa makosa 383 ambapo mwaka 2015 kulikuwa na makosa 2,976 yaliyoripotiwa kwa kipindi cha kuanzia januari hadi desemba ,tofauti na makosa yaliyoripotiwa 2016 ni 2,596.



Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amesema kuwa mafanikio ya mapungufu ya makosa ya kiuhalifu 383 ni sawa na asilimia 6.8%,na hii ni kutokana na juhudi za kila siku za jeshi la polisi,vyombo vya habari, pamoja na wananchi.


Amesema kuwa makosa makubwa ya kuwania mali ikilinganishwa na mwaka 2015,wizi wa silaha,ambapo yalikuwa makosa mawili,kipindi cha 2016 hakukuwa na tukio lolote la namna hiyo,makosa ya udanganyifu kwa kutumia silaha 2015 yalikuwa 56,ambapo mwaka 2016 yalikuwa 9 ni sawa na upungufu wa makosa  47.



Makosa ya wizi wa pikipiki mwaka 2015 yalikuwa 247 mwaka 2016 makosa 59 pungufu ya makosa 188 ambapo makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu 2015 yalikuwa 194 , mwaka 2016 yalikuwa makosa 70 hii pungufu ya makosa 124



Kamanda amesema kuwa Makosa ya wizi wa magari nayo yalipungua ambapo mwaka 2015 yalikuwa makosa 247 mwaka 2016 makosa 59 tofauti makosa 188,makosa ya wizi wa kuiba kwenye mabenki mwaka 2015 yalikuwa 56 mwaka 2016 hakukuwa na kosa lililoripotiwa,makosa ya uvunjaji wa nyumba  59 ambapo mwaka 2015 yalikuwa 900tofauti na mwaka 2016 yaikuwa makosa 841.



Makosa ya kuwania mali ambayo yaliongezeka ni kughushi ambapo mwaka 2015 kulikuwa na makosa 75 na mwaka 2016 yalikuwa makosa 93 sawa na ongezeko la makosa 6 ambapo jumla yalikuwa 47,makosa makubwa ya jinai nayo kwa asilimia kubwa yalippungua  ambapo makosa 64 yalitokea 2016 ikiwa ni pungufu ya makosa 13 huku makosa ya kubaka kwa mwaka
2015 yakiwa 170 tofauti na mwaka 2016 yalikuwa makosa 142 pungufu ya makosa 28


Makosa ya kulawiti katika 
kipindi cha mwaka 2015 
yalikuwa 48 ambapo  2016 makosa hayo 
yalipungua ahadi kufikia 41 ikiwa ni 
pungufu ya makosa 7,huku makosa ya kutupa 
watoto yalipungua kwa makosa 9 ambapo 2016yalikuwa 25. wakati 
huohuo makosa ya wizi wa watoto kulikuwa na ongezeko la 
makosa  2 ukilinganishwa na mwaka 2016 
,ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo takwimu zinaonyesha kulikuwa na 
makosa  4 tofauti na mwaka 2016 kulikuwa na makosa 
6.


Kamanda 
aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha mwaka 2016 ,makosa dhidi 
ya jamii yalipungua kutoka makosa 2,979 mwaka 2015 
hadi kufikia makosa 2,596 mwaka 2016.makosa hayo yapo kama ifuatavyo:kupakia 
silaha 2015 makosa 7,mwaka 2016 kosa lilikuwa 1,Nyara za serikali 2015 makosa 
30 mwaka 2016 makosa 17,kupatikana na magendo 2015 makosa 4,tofauti na mwaka 
2016  makosa 3.


Kamanda 
Chalers Mkumbo amesema kuwa katika hatua nyingine hali ya usalama barabarani 
mkoani Arusha 2016 ilizidi kuimarika tofauti na mwaka 2015,takwimu zinaonyesha 
kuwa mwaka 2015 kulikuwa na jumla ya ajali 85 tofauti na mwaka 2016 kulikuwa na 
ajali 70 ambapo upungufu ni ajali 15,Vifo vilikuwa 49 mwaka 2015 mwaka 2016 
vilikuwa 44 pungufu kwa makosa 5 hukun takwimu zikionyesha watu waliokufa kwa 
ajali hizo mwaka 2015walikuwa 54,tofauti na mwaka 2016 walikuwa 
50.


Aidha tozo za notification 
katika kipindi cha 
mwaka 2016 ziliongezeka hadi kufikia 4,708,680,000 (bilioni nne 
milioni mia 
saba na nane laki sita na elfu themanini)tofauti na mwaka 2015 ambapo jumla 
yake ilikuwa shilingi 3,227,640,000(bilioni tatu milioni mia 
mbili ishirini na 
saba laki sita na elfu arobaini

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages