PETER aliangalia namna ambavyo Baba yake alivyokuwa akikunja uso wakati akimeza kile chakula kilichokuwa kimejaa chumvi. Alimuangalia na mkewe namna alivyokuwa akila kwa wasiwasi akiona aibu kuwa chakula chake cha kwanza kupika ukweni kilikuwa kikilika kwa shida. Huku akitabasamu Peter alinyanyua kichwa na kumuangalia mkewe kisha kwa sauti ya juu alisema.
"Honey naomba chumvi kidogo." Kila mtu alinyanyua kichwa kwa mshtuko kusikia kuwa pamoja na kujaa kwa chumvi ile bado alidai kuongeza.
"Ndiyo, chumvi, aliongea huku akimkodolea mcho mkewe na kumkonyeza kidogo." Mkewe alielewa na kunyanyuka kwenda kumletea chumvi watu wote kwenye meza waliacha kula na kumuangali. mkewe alimletea na kuichukua akaongeza kwenye wali kwa kunyunyuzia chumvi ya kutosha, kisha akaanza kula huku akitabasamu, alijikaza sana kutokuonyesha kuwa alikuwa akiumia kwa chumvi nyingi.
"Yaani wewe na chumvi yako, unanifanya na mimi naanza kupenda chumvi...nisije kuwa kama wewe." Mkewe aliongea huku na yeye akichukua chumvi na kunyunyuzia kidogo.
"Si ndiyo vizuri, au hutaki tufanane?" Peter alitania watu wote pale kwenye meza walitingisha tu vichwa huku wakiwashangaa jinsi wanavyokula. Waliacha kuwaza namna chakula kilivyokuwa na chumvi na kuwaza namna ambavyo Peter alikuwa anapenda chumvi.
*****
Funzo; Yabebe mapungufu yote ya mkeo kwa wazazi na ndugu zako wewe na yeye akusaidie kubeba mapungufu yako kwa wazazi wake. Hii inatokana na ukweli kuwa ni rahisi wao kumchukia mkeo kwakuwa si ndugu yao kuliko kukuchukia wewe. hivyo hivyo upande wa mkeo, hawawezi kumchukia Binti yao kwa vitu vizogo lakini wewe wanaweza kukuchukia.
Acha tabia ya kumzungumzia vibaya mwenza wako hata kama ni kwa utani, kila wakati kuwa tayari kumlinda na mkifika chumbani ndiyo unamuambia ukweli. haitakusaidia kitu kama marafiki zako wote, ndugu au mashoga zako watamchukia mkeo au mumeo kwa maneno uliyowaambia hata kama ni ya ukweli. Mlinde kwaajili ya kumtunzia heshima.
Wanandoa chukua yako hapo
*Nimeitoa Mahali..
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)