Meneja usalama ,afya na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda,(wa pili kulia) akiwakabidhi zawadi za opena za safari wafanyakazi wa Tbl Group wakati wa Uzinduzi wa promosheni ya Safari kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa hafla wa uzinduzi wa Promosheni mpya ya Safari iliyofanyika Ilala jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa TBL Group Msigwa Sepoko akikabidhiwa zawadi yake ya begi la Safari na Balozi wa Safari, Getrude Francis (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni ya Safari kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo iliyofanyika Ilala jijini Dar es Salaam
Balozi wa bia ya Safari Getrude Francis (kulia) akikabidhi zawadi ya begi la Safari kwa mfanyakazi wa TBL Group Msigwa Tina Kimalia wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni ya Safari kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo iliyofanyika Ilala jijini Dar es Salaam
Wafanyakazi wakijizolea zawadi za promosheni
Kampuni ya TBL Group inatarajia kuzindua promosheni kubwa ya kunufaisha wateja wake kupitia bia yake maarufu ya Safari Lager.Kabla ya uzunduzi kwa wateja wa nje imezindua promosheni hiyo kwenye viwanda vyake vilivyopo jijini Dar es Salaam na mikoa mbalimbali ambapo wafanyakazi walifurahia kinywaji hicho wakati huohuo baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali baada ya namba zao kushinda katika droo ndogo ya ndani ya uzinduzi wa promosheni kwa wafanyakazi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)