Wafanyakazi wakiwa wanaburudika wakisheherekea kupata tuzo na NOSA
Wafanyakazi wakipongezana kutokana na mafanikio ya kampuni ya kushinda tuzo ya NOSA
Wakipata burudani ya muziki kusheherekea mafanikio hayo.
Viwanda cha kutengeneza vinywaji vya TBL Dar es Salaam na TBL Mbeya vimepata tuzo ya utekelezaji kanuni za Usalama na Afya mahali pa kazi kutoka shirikisho la kimataifa la kusimamia masuala ya usalama mahali pa kazi lenye makao makuu nchini Afrika ya Kusini lijulikanalo kama National Occupational Safety Association (NOSA).
Tuzo hii ambayo viwanda vya TBL Group vya Mbeya,Mwanza na Dar es Salaam vimeipata mfululizo imekuwa ikitolewa kutokana na kukidhi viwango vya kimataifa vya utekelezaji kanuni za afya,usafi na usalama mahali pa kazi ambapo wataalamu kutoka taasisi ya NOSA wamekuwa wakija nchini kufanya ukaguzi kwenye viwanda vyake na vimekuwa vikipata alama ya kufanya vizuri kwenye kiwango cha nyota nne na nyota tano.
Akiongea wakati wa hafla ya kusherehekea tuzo hiyo mwishoni iliyofanyika katika kiwanda cha Ilala,Meneja wa kiwanda cha TBL cha Dar es Salaam,Calvin Martin alisema kuwa kampuni inajivunia kuendelea kufanya vizuri katika suala la Usalama na Afya mahali pa kazi ambapo mwaka huu imeshinda kwa kiwango cha nyota tano ambacho ni kiwango cha ufanisi cha hali ya juu
“Tunayo sababu ya kusherehekea kupata tuzo hii tena katika kipindi cha mwaka huu kwa kuwa inadhihirisha kuwa kampuni inajali suala la usalama na afya kwa wafanyakazi na hili ni jambo la msingi kwa kuwa usalama na Afya ukikosekana mazingira yetu ya kufanyia kazi yatakuwa hatarini na ufanisi hautakuwepo”.Alisema.
Aliwapongeza wafanyakazi wote kwa jinsi wanavyoshiriki kuzingatia kanuni na miongozo inayowekwa na kampuni hali ambayo inachangia kuleta mafanikio na kuvifanya viwanda vilivyopo chini ya TBL Group kuongoza kufanya vizuri na kuwa mfano wa kuigwa na viwanda vingine nchini.
Kwa upande wake Meneja wa Usalama na Afya kwa TBL,Renatus Nyanda,amesema kuwa kampuni imeweka mikakati kuhakikisha viwanda vyake vyote vinatekeleza kanuni za Afya na Usalama kwa viwango vya kimataifa na ndio maana inaendelea kupata tuzo hizi za Usalama kuazia zinazotolewa na taasisi za hapa nchini na nje ya nchi “Leo tunaposheherekea kupata tuzo hii wenzetu wa Mbeya nao wanasheherekea na ukaguzi unaendelea katika viwanda vingine”.Alisema
Alitoa wito kwa wafanyakazi wote wa viwanda vya TBL Group kuendelea kutekeleza miongozo mbalimbali ya utendaji wenye kuleta ufanisi ili waendelee kuwa kioo hususani katika suala hili la usalama na Afya kwa kuwa linawagusa moja kwa moja katika maisha yao ya kila siku.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)