Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msanii Ali Kiba ambaye atakuwepo kutumbuiza na kutoka kulia ni Msanii Madee pamoja na Meneja Mauzo wa Huawei, Bw. Zhang Heng, ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
Msanii wa muziki wa bongo flava Ali Kiba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Wakimsikiliza kwa makini kulia ni Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li na kushoto ni Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian. Huawei ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
Msanii wa bongo flava kutoka kundi la TipTop Connenction lenye maskani yake Manzese, Madee akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Huawei ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
Msanii wa kizazi kipya Bi. Snura alimaarufu ‘Mama Majanga’ akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Huawei ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
Msanii wa muziki wa singeli Eskide akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian. Huawei ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL.
Kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa Huawei, Bw. Zhang Heng, ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la StarTimes Kiswahili linalokwenda kwa jina la SEREBUKA MUSIC FESTIVAL, Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes Tanzania, Bw. Damien Li, Msanii wa muziki wa bongo flava Ali Kiba na Meneja wa chaneli ya StarTimes Swahili, Bi. Wang Qian wakikata keki kuashiria uzinduzi wa tamasha la kusherehekea miaka miwili ya chaneli ya Kiswahili ya StarTimes litakalofanyika siku ya Jumamosi Agosti 13, 2016 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog.
Tamasha
hilo litafanyika siku ya Jumamosi, Agosti 13, 2016 katika viwanja vya posta
Kijitonyama.
·
Wasanii
wakubwa nchini kulishambulia jukwaa, wakiwemo Ali Kiba, Lady Jaydee, Yamoto
Band, Madee, Juma Nature, Snura, Stamina, Eskide (msanii wa muziki wa singeli)
na bila ya kusahau wakali wa bongo movie pia watakuwepo.
·
Watanzania
wataweza kujionea jukwaani vipindi mbalimbali vinavyorushwa kupitia chaneli
hiyo inayoonekana hapa nchini Tanzania na Kenya.
Dar es Salaam, Agosti 1, 2016. Wasanii wa muziki wa Bongo Flava
Ali Kiba na Lady Jaydee wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la kusherehekea
miaka miwili tangu kuanzishwa kwa chaneli ya StarTimes Kiswahili siku ya
Jumamosi ya Agosti 13, 2016 katika viwanja vya Posta, Kijitonyama.
Akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na tamasha hilo Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na Maudhui wa StarTimes
Tanzania, Bw. Damien Li amesema kuwa tamasha hilo linadhamiria kusherehekea kwa
pamoja na wateja wao mafanikio yaliyofikiwa na chaneli ya StarTimes Kiswahili
katika kuonyesha vipindi vyenye maudhui ya Kiswahili nchini Tanzania na Kenya.
“Chaneli hii mwaka huu mwezi wa
Agosti inatimiza miaka miwili tangu kuanzishwa kwake mnamo Agosti mosi mwaka
2014. Chaneli ya StarTimes Kiswahili inaonekana katika nchi mbili za Tanzania
na Kenya na hivyo kutoa wigo mpana kwa wasanii na watayarishaji wa vipindi hapa
nchini kupata fursa ya kuonekana maeneo hayo. Vipindi vingi katika chaneli hii
huangazia masuala ya filamu, muziki, burudani, vyakula, mitindo ya maisha na
mavazi pamoja na tamaduni za watu wa Afrika ya Mashariki hususani kwa nchi hizo
mbili ambavyo huwasilishwa kwa lugha ya Kiswahili.” Alisema Bw. Li
“Tamasha hili litahusisha shughuli
mbalimbali hususani kuangazia maudhui yanayopatikana kwenye chaneli ya
StarTimes Kiswahili lakini pia litapambwa na burudani kadhaa kutoka kwa wasanii
watakaoalikwa. Siku hiyo watanzania watawashuhudia wasanii wakubwa wa muziki wa
bongo flava jukwaani kama vile Ali Kiba, Lady Jaydee, Juma Nature, Madee, Yamoto
Band, Snura na Stamina. Pia kutakuwepo na wasanii mashuhuri kutoka katika
tasnia ya bongo movie ambao filamu zao zinaonekana kupitia chaneli hii kama
vile Wema Sepetu, JB, Steve Nyerere na Ray Kigosi.” Aliongezea Bw. Li
Chaneli ya StarTimes Kiswahili inapatikana
katika visimbuzi vyote viwili vya StarTimes yaani cha antenna kuazia kifurushi
cha NYOTA kwa shilingi 6000/- na cha dishi kuanzia kifurushi cha NYOTA PLUS kwa
shilingi 8000/- kama malipo ya mwezi. Kampuni hiyo inajivunia kuwa ya kipekee
nchini Tanzania kwa kutoa matangazo bora ya dijitali kwa gharama nafuu ambayo
kila mtu anaweza kuimudu.
“Ningependa kutoa wito kwa wateja
wa StarTimes na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika tamasha hili
litakalofanyika siku ya Jumamosi ya Agosti 13 mwaka huu pale viwanja vya Posta,
Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Tiketi zitapatikana kwa bei ya kawaida kabisa
ya kuanzia shilingi 5000/- na kupatikana katika vituo vitakavyoanza kutangazwa
kwa njia mbalimbali. Tamasha hili ni maalumu kwa ajili ya kuwashukuru
watanzania kwa kuipokea vizuri chaneli hii na kuifanya kuwa chaguo lao kubwa
pindi watazamapo luninga, hivyo naomba wajitokeze kwa wingi.” Alimalizia Bw. Li
Naye kwa upande wake msanii wa
bongo flava Ali Kiba akizungumza mbele ya waandishi wa habari amewaahidi
makubwa wateja wa StarTimes na watanzania watakaohudhuria siku hiyo kuwa
watapata burudani ya aina yake.
“Kwanza kabisa ningependa kutoa
pongezi za dhati kwa kampuni ya StarTimes kwa kutambua mchango wa lugha ya
Kiswahili na kuikuza miongoni mwa nchi wanazofanya biashara. Hii ni fursa ya
kipekee kwa wasanii na watayarishaji wa kitanzania kuweza kupanua wigo wa kazi
zao na kuweza kuonekana sehemu zingine. Kusema ukweli hapo awali wakati
matangazo ya dijitali yanaingia nchini sikuweza kuiona fursa hii lakini sasa
ninaona kazi za wasanii wetu zinaonekana na kutambulika kimataifa.” Alisema Ali
Kiba
“Ningependa kutoa wito kwa
StarTimes kupanua wigo zaidi wa chaneli hii ifike katika nchi zingine za jirani
kama vile Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Kongo hata Afrika ya Kusini kwani
kuna watanzania kule na waafrika ambao wanapenda kufahamu lugha ya Kiswahili na
tamaduni za waswahili wenyewe. Na mwisho kabisa ningependa kuwaalika watanzania
wote siku hiyo waweze kuhudhuria kwa wingi kwani tamasha hili ni lao, nawaomba
waje kwa wingi kusherehekea kwa pamoja maudhui mazuri na ya kusisimua
yanayopatikana ndani yake.” Alihitimisha Ali Kiba au King Kiba kama
anavyojulikana miongoni mwa mashabiki wake
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)