Pages

ZLATAN IBRAHIMOVIC ATUA OLD TRAFFORD


Manchester United itakamilisha usajili wa Zlatan Ibrahimovic na huenda dili hilo likakamilika kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2016, taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Sky Sports.
Inaeleweka kwamba, kaimu mtendaji mkuu wa United Ed Woodward na wakala wa Ibrahimovic wanamalizia makubaliano ya uhamisho wa mkataba wa mwaka mmoja, Jose Mourinho anataka kufanya usajili wa nyota huyo wa Sweden kuwa usajili wake wa kwanza tangu atue Old Traffoed.
Uhamisho huo huru unatokana na kumalizika kwa mkataba wa Ibrahimovic na Paris Saint-Germain hivi karibuni na dili hilo linatarajiwa kukamilika kabla ya mchezo wa kwanza wa Kundi E kati ya Sweden dhidi ya Ireland  unaotarajiwa kuchezwa June 13.
Vyanzo vya Sky vinaamini Ibrahimovic ndiye striker pekee ambaye Mourinho anamtaka katika usajili wa majara haya ya joto, Mreno huyo ameshawishiwa na Marcus Rashford na kuamini safu yake ya ushambuliaji itakuwa tishio msimu ujao.
Wakati Mourinho akiamini Ibrahimovic ni mchezaji muhimu ambaye United inamuhitaji kama inataka kuwania taji la Premier League msimu ujao, pia yupo makini kuhakikisha anampa nafasi ya kutosha Rashford kuendeleza kasi yake.
Taarifa kutoka Sky Sports zinadai kwamba, Mourinho anatambua na anataka kuendeleza utamaduni wa United wa kuwapa nafasi vijana kwenye kikosi cha kwanza na aliachana na kumsajili striker wa Leicester Jamie Vardy wiki hii ili kulinda kipaji cha Rashford.
Vyanzo vya Sky Sport awali viliripoti United kuvutiwa na mchezaji huyo wa zamani wa Malmo FF, Ajax, Juventus, Inter Milan, Barcelona na AC Milan tangu mapema mwezi May wakati Mourinho akitangazwa kurithi nafasi ya Louis van Gaal.
Mazungumzo kati ya United na wakala wa Ibrahimovic Mino Raiola yalishika kasi baada ya Mourinho kutua Old Trafford, na vyanzo vya Sky Sports mara kadhaa wiki iliyopita viliripoti kwamba, walikuwa klabu pekee ya Premier League ambayo Ibrahimovic alikuwa akiitazama.
Ieleke kwamba, nyota huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 5 mzaliwa wa Malmo swedem, anataka kuongeza kikombe kutoka ligi ya EPL ambapo tayari amesha twaa ndoo kwenye ligi za Spanish La Liga, Italian Serie A, French Ligue 1 na Dutch Eredivisie.
Ibrahimovic alikuwa akiwaniwa kwa madau makubwa kutoka vilabu vya Super League ya China lakini imetokea ameshawishika kuelekea Manchester United kuungana na Mourinho.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)