Licha ya Taifa Stars kupoteza mchezo wake dhidi ya timu ya Taifa ya Misri watanzania wengi walikuwa wamejitoa kwa kila hali kuishangilia katika mchezo huu wa nyumbani uliokuwa unafuatiliwa kwa karibu na wapenzi wa soka nchini kote.
Katika kuhakikisha wachezaji wa Taifa Stars wanaongezewa hamasa ya kucheza kwa kushangiliwa, kampuni ya TBL Group ambayo ni mmoja wa wadhamini wa timu ya taifa mwishoni mwa wiki iliwawezesha baadhi ya wafanyakazi wake ,familia zao na baadhi ya mawakala wa kuuza bidhaa zake kuangalia mpambano wa Taifa Stars na timu ya taifa ya Misri.
Lengo kubwa la kuwapatia tiketi za mchezo wafanyakazi wake na baadhi ya wateja lilikuwa ni kuiongezea nguvu Taifa Stars kwa kuishangilia.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa na msisimko mkubwa na kuwavutia maelfu ya washabiki wa soka nchini Taifa Stars ilifungwa mabao 2-0 na timu ya Misri ‘The Pharaohs’
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)