Wakazi wa Kata ya Muriet jiji la Arusha wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda. |
Mratibu wa Tasaf Jiji la Arusha,Tajiel Mahega akisoma taarifa kabla Kaya zilizotambuliwa kukabidhiwa rasmi. |
Sehemu ya Kuku wa kienyeji waliokabidhiwa wananchi kutoka Kaya masikini. |
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Daudi Felix Ntibenda ametos wito kwa wananchi wa Kata ya Murieti kuhakikisha wanajenga Shule ya Sekondari ili kusogeza huduma hiyo kwa wanafunzi wa maeneo hayo wanaotembea umbali mrefu kufuata shule.
Wito huo ameutoa juzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa ufugaji wa Kuu wa asili (Kienyeji ) na Mbuzi wa Maziwa kwa kaya 85 za Mtaa wa Terrat Mlimani katika Jiji la Arusha kupitia Mradi wa TASAF III unaofadhiliwa na Umoja wa Nchi zinazozalisha Mafuta (OPEC).
Katika uzinduzi huo Ntibenda aliwahimiza wananchi hao kutafuta eneo linalofaa kujengwa Shule hiyo,kisha Mstahiki Meya wa Jiji kwa kushirikiana na Diwani kuitisha harambee ya kuchangia ujenzi wa Shule ya Sekondari katika Kata hiyo.
Pia aliwasihi wananchi kuwa makini na mradi huu wa Ufugaji ili uweze kuinua kipato na kuboresha maisha ya wakazi wa Terrati Mlimani na maeneo mengine ambayo yametambuliwa kuwa ni masikini.
Mtaa huu ni mojawapo kati ya mitaa 70 ya Jiji la Arusha inayonufaika na uhawilishaji wa Fedha kunusuru Kaya masikini ambapo kila baada ya miezi miwili hupokea jumla ya Tsh 3,182,000 kwa ajili ya kaya zilizoko kwenye mradi.
Akizungumza katika hafla hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro aliwawapongeza Menejimenti ya Jiji kwa kusimamia zoezi zima la Uhawilishaji wa Fedha kwa masikini kwa kuwalenga wananchi wale wenye kipato cha chini kama ilivyo malengo ya mradi huu.
Mwishoni mwa mwaka 2015, Halmashauri ya Jiji iliomba Fedha zaidi ya Milioni mia tatu kutoka Tasaf kwa ajili ya utekelezaji wa miradi Tisa ambayo ni Ujenzi wa madarasa 2 Shule ya Msingi Azimio,Ujenzi wa Bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Korona, na kwenye maeneo yenye uhaba wa chakula .
Miradi itakayotekelezwa ni Ujenzi wa Kivuko Mtaa wa Oloresho, upandaji wa miti na miche mtaa wa Ally Nyanya pamoja na upandaji wa miti na miche mtaa wa Osunyai.
Pia mradi huu haukusahau makundi maalumu kama Ushonaji eneo la Kambi ya Fisi, Ufugaji wa Kuku wa kienyeji eneo la Moivio , Mradi wa Kuku wa kienyeji na Mbuzi Terrati Mlimani na mradi wa ufugaji wa Kuku wa kienyeji eneo la Lolovono.
Mpaka sasa Halmashauri imepokea jumla ya Tsh 74 milioni kwa ajili ya kununua Kuku, Mbuzi na kutoa chakula, madawa kwa kipindi cha miezi sita katika Mtaa wa Terrati Mlimani, Lolovono pamoja na Moivoi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)