Siku ya Familia TBL Mwanza 2016 burudani tele - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Siku ya Familia TBL Mwanza 2016 burudani tele

 Wafanyakazi na familia zao walipata burudani za muziki ,maakuli na vinywaji
 Watoto wa wafanyakazi waliburudika kwa michezo mbalimbali
Wafanyakazi wa kampuni ya Bia ya TBL Mwanza wameungana na familia zao katika sherehe za familia zilizofanyika katika viwanja vya hoteli ya Ndorosi iliyopo jijini humo.
 Akizungumza katika sherehe hizo, Meneja wa Kiwanda cha Mwanza, Richmond Raymond amesema lengo la siku hiyo ya Siku ya Familia ni kukutanisha wafanyakazi nje ya mazingira ya kazi na kukutana pamoja na kufurahi wakiwa na familia zao .
Amesema Wafanyakazi mara nyingi hukutana wakiwa kazini lakini watoto, wake na waume zao hawafahamiani hivyo kupitia siku ya familia husaidia kujenga uhusiano na kufanya kuwa familia moja.
Pia alitumia fursa hiyo kuwapongeza wafanyakazi wenzake kwa kazi nzuri wanayofanya katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuwataka wazidishe bidii zaidi ili kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji.

Siku hiyo ilikuwa na burudani za kila aina kuanzia michezo,burudani za watoto na watu wazima bila kusahau vinywaji na maakuli ya kukata na shoka




No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages