Katika kusherekea siku maalum ya mtoto wa Afrika ambayo hufanyika Juni, 16 ya kila mwaka, Kamati ya Miss Universe Tanzania kupitia mpango wake mpya uitwao Binti Jasiri ilikutanisha kwa pamoja watoto 90 kutoka vituo mbalimbali vya mkoa wa Dar es Salaam ambapo halfa hiyo ilihudhuliwa na Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot na mgeni rasmi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akizungumza na watoto hao, Makonda aliwambia kuwa serikali ya awamu ya tano inawathamini watoto na hata kuwawekea elimu bure hivyo waongeze juhudi katika masomo yao ili nao waweze kuja kuwa na maisha mazuri na hata kuwasaidia wengine kama jinsi wao wanavyosaidiwa na watu wengine ambao wamefanikiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na watoto kutoka vituo mbalimbali vya kulea watoto kutoka mkoa wa Dar es Salaam katika halfa maalum ya kusherekea siku ya mtoto wa Afrika, Kushoto ni Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)
“Watu wenye maisha mazuri wasiwachanganye hata nyie mnaweza kuwa na maisha mazuri hata zaidi yao, mnatakiwa muongeze bidii katika masomo yenu ili na nyie mfanikiwe na kuwasaidia wenzenu kama jinsi mnavyosaidiwa na wengine kwa sasa,” alisema Makonda.
Nae Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot ambaye pamoja na kupata chakula cha pamoja na watoto hao pia alipata nafasi ya kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu maisha, kuwashauri na kuwatia moyo ili waongeze bidii katika masomo yao na hata baadae waweze kufanikiwa kimaisha.
Halfa hiyo ilisimamiwa na Magdalena Gisse na kuhudhuliwa na watoto kutoka Kituo cha Malaika Kids Orphanage, Kurasini Orphanage, Sarafina Orphanage na Makini Orphanage vyote kutoka mkoa wa Dar es Salaam.
Na Rabi Hume, MO Blog
Watoto wakimpigia makofi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumaliza kuzungumza nao katika halfa maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimsalimu mmoja wa watoto waliohudhulia halfa maamul ya kumkumbuka mtoto wa Afrika, Aliyembeba mtoto huyo ni Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot na katikati ni Mkurugenzi Kitaifa wa Miss Universe Tanzania, Maria Sarungi Tsehai.
Watoto mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo wakifurahi kwa pamoja.
Baadhi ya watoto waliohudhuria halfa hiyo walio na imani ya Kiislamu wakisali.
Meneja wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzalez akifuturu kwa pamoja na watoto kutoka vituo mbalimbali waliohudhuria halfa maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika.
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akifuturu kwa pamoja na watoto waliohudhuria katika siku maalum ya kumbukumbu ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip.
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akimlisha mmoja wa watoto waliohudhuria halfa maalum ya kumkumbuka mtoto wa Afrika.
Watoto mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo wakifuturu na kujiburudisha na vinywaji kutoka Kampuni ya Mohammed Enterprises ambayo ilijitolea vinywaji katika halfa maalum ya kumkumbuka mtoto wa Afrika.
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akiwa katika picha ya pamoja na watoto waliohudhuria halfa hiyo.
Meneja wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzalez akifurahi na watoto waliohudhuria halfa hiyo kwa kuwaonyesha jinsi mtandao wa kijamii wa Snapchat jinsi unavyotumika.
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akizungumza na watoto waliohudhuria halfa hiyo.
Mmoja wa watu waliokulia katika kituo cha kulelea watoto cha DogoDogo, Dk. Yusuph akiwatia moyo watoto hao na jinsi ambavyo wanaweza kufanya ili na wao waweze kufanikiwa kama ilivyo kwake.
Msimamizi wa halfa hiyo, Magdalena Gisse akiwashukuru watoto waliohudhuria halfa hiyo.
Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akiwasaidia watoto kufungua maputo baada ya halfa hiyo kumalizika.
Meneja wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzalez akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto waliohudhuria halfa maalum ya kumkumbuka mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip.
Washiriki wa halfa maalum ya mtoto wa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)